• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali na Majibu |
    • Barua pepe |
Tanga Region
Tanga Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Tanga

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Dira na Dhima
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za maji
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
    • Idara
      • Utawala na Utumishi
      • Mipango na Uratibu
      • Miundombinu
      • Elimu
      • Afya
      • Maji
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Usimamizi wa Serikali za Mitaa
    • Vitengo
      • TEHAMA
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa ndani
      • Manunuzi
      • Sheria
  • Machapisho
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu za Maombi
    • Hotuba
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Sehemu ya picha
    • Habari
    • Matukio
  • Miradi
    • Miradi iliyokamilika
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya Pangani
    • Halmashauri ya Wilaya Mkinga
    • Halmashauri ya Wilaya Muheza
    • Halmashauri ya Jiji Tanga
    • Halmashauri ya Wilaya Korogwe
    • Halmashauri ya Mji Korogwe
    • Halmashauri ya Wilaya Handeni
    • Halmashauri ya Mji Handeni
    • Halmashauri ya Wilaya Kilindi
    • Halmashauri ya Wilaya Lushoto

WATOKA NYUMBANI 'PATUPU', WAREJEA NA MILIONI 3, MAJIKO YA GESI YA RC TANGA

Imewekwa tarehe: May 26th, 2025

Na Mashaka Mgeta, OMM TANGA

DHANA ya msemo wa ’mtembea bure si sawa na mkaa bure, huenda akaokota’ imedhihirika leo Mei 26, 2025 kwa baadhi ya wanawake wa kijiji cha Kilulu Duga, wilaya ya Mkinga mkoani Tanga.

Ingawa ’hawakutoka bure’ nyumbani kwao, walikwenda katika zahanati ya kijiji hicho kunapojengwa wodi ya mama mtoto, kushiriki ziara ya Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Mhe Balozi Dkt Batilda Burian, aliyefuatana na wajumbe wa Kamati ya Usalama (KU) kukagua mradi huo wenye thamani ya Shilingi milioni 35, utakaopitiwa na Mwenge wa Uhuru 2025.

Wanawake hao, Mwanaidi Mwaboga, Pili Makau, Fatuma Kikoya, Saumu Makau, Mwanaidi Hassan na Mariam Mzinga, wametakiwa kuunda kikundi na kubuni mradi wenye thamani ya kati ya Shilingi milioni 2 na milioni 3, kutoka kwa Mhe Balozi Dkt Batilda.

Pia, Mhe Balozi Dkt Batilda, ametoa majiko ya gesi kwa wanawake hao, kama ishara ya kuunga mkono mkakati wa matumizi ya nishati safi ya kupikia unaosimamiwa na Mhe Rais Dkt Samia Suluhu Hassan, na kutekelezwa kwenye mataifa mbalimbali barani Afrika.

Mmoja wa wanawake hao, Pili Makau, amesema msaada wa fedha hizo utawainua kukuza uwezo wao wa uzalishaji bidhaa za kufuma, na kuyafikia masoko hasa yaliyopo jijini Tanga.

Naye Said Kibwana, mkazi wa kijiji hicho, alisema hatua hiyo ni yenye kuungwa mkono kwa viongozi wengine kuwa wasaidizi na wawezeshaji wa wananchi wanaohitaji kukua kiuchumi.

Kijana Mwikeni Omar, amesema ni miongoni mwa walionufaika na mkopo wa bodaboda kutoka kwenye Halmashauri ya Wilaya ya Mkinga, hivyo kuwapa matumaini wanawake hao kuwa, fedha watakazopokea zitabadilisha maisha yao.

Mwenge wa Uhuru 2025 wenye kauli mbiu inayosema ”Jitokeze kwa wingi Kushiriki Uchaguzi Mkuu 2025 kwa amani na utulivu’, unatarajiwa kuwasili na kukimbizwa mkoani Tanga kuanzia Juni 6 hadi 17, mwaka huu.

Matangazo

  • MATOKEO YA MTIHANI WA KIDATO CHA NNE (CSEE)2023 January 25, 2024
  • HOTUBA YA MKUU WA MKOA WA TANGA MHE. WAZIRI WAZIRI KINDAMBA KATIKA HAFLA YA UFUNGUZI WA KONGAMANO LA UWEKEZAJI NA UZINDUZI WA MWONGOZO WA FURSA ZA UWEKEZAJI MKOA WA TANGA 16/11/2023 November 27, 2023
  • FORM ONE SELECTION 2024 December 20, 2023
  • TANGA REGION INVESTMENT GUIDE November 24, 2023
  • Angalia zote

Habari mpya

  • UTENZI: KARIBU MWENGE WA UHURU MKOANI TANGA - JULAI 6, 2025

    May 31, 2025
  • TAHADHALI: ASILIMIA 60 YA UBORA WA NGOZI INAPOTEA KWENYE KUCHUNA

    May 29, 2025
  • TANGA WAASWA KUENDELEZA UKAGUZI, UTUNZAJI MIRADI BAADA YA MWENGE WA UHURU

    May 29, 2025
  • WATOKA NYUMBANI 'PATUPU', WAREJEA NA MILIONI 3, MAJIKO YA GESI YA RC TANGA

    May 26, 2025
  • Angalia zote

Video

KATIBU TAWALA MKOA WA TANGA AKIONGOZA WATUMISHI WA MKOA HUO KUFANYA MAZOEZI YA PAMOJA KATIKA UWANJA WA MKWAKWANI KUITIKIA WITO WA MHE. MAKAMU WA RAIS
Video zaidi

Viunganishi vya haraka

Tovuti zinazoendana

  • TAMISEMI
  • Kupata huduma za kiutumishi
  • Wakala ya Serikali Mtandao
  • Utumishi
  • Baraza la Mitihani Tanzania (NECTA)
  • Tovuti ya Serikali

Kifuatilia watazamaji duniani

world map hits counter

idadi ya watazamaji

free HitCounter

Ramani ya Mkoa wa Tanga

Wasiliana nasi

    Golf Area/Masiwani Road Tanga

    Anuani ya posta: P.O.Box 5095 Tanga

    Simu: 027 2642421

    Simu ya Mkononi:

    Barua pepe: ras.tanga@tamisemi.go.tz

Anuani zingine

   

    • Sera za faragha
    • Kanusho
    • Maswali na Majibu
    • Ramani ya Tovuti
    • Huduma

Haki miliki ©2017 Katibu Tawala Mkoa wa Tanga . Haki zote zimehifadhiwa.