Na Mashaka Mgeta, LUSHOTO
VIONGOZI wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) mkoani Tanga, wametakiwa kuepuka hulka za ‘kinyampala’ wakati wa kukagua miradi ya maendeleo inayotekelezwa na Serikali.
Katibu wa CCM wa Mkoa wa Tanga, Mfaume Kizigo, amesema hayo alipoongoza baadhi ya wajumbe wa Kamati ya Siasa ya chama hicho mkoani humo, kukagua miradi ya maendeleo kwenye halmashauri za wilaya za Lushoto na Bumbuli leo Mei 15, 2025.
Amesema, ukaguzi unaofanywa na Chama hicho ni sehemu ya nia yake, kujiridhisha na hatua mbalimbali za utekelezaji wa miradi husika, ili kutoa taarifa kwa wananchi walioikubali Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya 2020 – 2025, na kukipa dhamana ya uongozi wa nchi.
Kizigo amesema, dhana ya Chama kuisimamia Serikali imejikita katika ushiriki wa viongozi na wanachama wake na kuwa mfano wa kuigwa katika shughuli za maendeleo.
Amesema baada ya ukaguzi wa miradi hiyo, Kamati ya Siasa ya Mkoa imeridhishwa na hatua zilizofikiwa kwa miradi ya ujenzi wa Shule ya Amali ya Shita, ujenzi wa madarasa mawili na matundu sita ya vyoo katika Shule ya Msingi Mabhughai na bweni la wasichana kwenye Shule ya Sekondari ya Wasichana Kwalei wilayani Lushoto.
Kizigo amesema, ubora wa miundombinu iliyojengwa wilayani humo ni ishara ya matumizi sahihi ya fedha kwa thamani yake, na usimamizi bora wa Mkuu wa Wilaya ya Lushoto, Mhe Sumaye.
Golf Area/Masiwani Road Tanga
Anuani ya posta: P.O.Box 5095 Tanga
Simu: 027 2642421
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ras.tanga@tamisemi.go.tz
Haki miliki ©2017 Katibu Tawala Mkoa wa Tanga . Haki zote zimehifadhiwa.