• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali na Majibu |
    • Barua pepe |
Tanga Region
Tanga Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Tanga

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Dira na Dhima
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za maji
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
    • Idara
      • Utawala na Utumishi
      • Mipango na Uratibu
      • Miundombinu
      • Elimu
      • Afya
      • Maji
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Usimamizi wa Serikali za Mitaa
    • Vitengo
      • TEHAMA
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa ndani
      • Manunuzi
      • Sheria
  • Machapisho
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu za Maombi
    • Hotuba
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Sehemu ya picha
    • Habari
    • Matukio
  • Miradi
    • Miradi iliyokamilika
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya Pangani
    • Halmashauri ya Wilaya Mkinga
    • Halmashauri ya Wilaya Muheza
    • Halmashauri ya Jiji Tanga
    • Halmashauri ya Wilaya Korogwe
    • Halmashauri ya Mji Korogwe
    • Halmashauri ya Wilaya Handeni
    • Halmashauri ya Mji Handeni
    • Halmashauri ya Wilaya Kilindi
    • Halmashauri ya Wilaya Lushoto

DK MPANGO: MITAMBO MIWILI YA JNHPP KUWASHWA MWEZI UJAO

Imewekwa tarehe: February 21st, 2024

DK MPANGO: MITAMBO MIWILI YA JNHPP KUWASHWA MWEZI UJAO

Na Mashaka Mgeta na Zuberi Mgaya, HANDENI

MAKAMU wa Rais, Mhe Dk Philip Mpango, amesema mitambo miwili iliyopo kwenye bwawa la kuzalisha umeme la Mwalimu Nyerere (JNHPP), itawashwa mwezi ujao wa Machi mwaka huu, ikiwa ni sehemu ya jitihada za kukabiliana na upungufu wa nishati hiyo nchini.

Mhe Dk Mpango amesema hayo leo alipokuwa akizungumza na wananchi wa wilaya ya Handeni kwenye eneo la Kabuku, akiwa katika siku ya kwanza ya ziara yake ya siku tatu mkoani Tanga.

Kauli ya Mhe Dk Mpango ilitanguliwa na hoja ya Diwani wa Kata ya Kabuku Ndani wilayani Handeni, Mhe Abdallah Pendeza, kuainisha changamoto mbalimbali zinazoikabili kata hiyo ikiwemo mgawo wa umeme.

Mhe Dk Mpango amesema, awali, Serikali inayotekeleza mipango ya kitaifa na inayohusu maeneo mahususi kukabiliana na upungufu wa umeme, ilipanga kuwasha mtambo mmoja kuongeza umeme kwenye gridi ya taifa,  lakini iliahirishwa na badala yake itawashwa mitambo miwili mwezi ujao.

Kuhusu hatua mahususi za kupunguza changamoto ya hiyo kwenye baadhi ya maeneo mkoani Tanga, Mhe Dk Mpango amesema Serikali inajenga kituo cha kupozesha umeme katika kata ya Mkata wilayani Handeni, hivyo wananchi wanatakiwa kuwa na subira wakati mradi huo ukitekelezwa.

Mhe Dk Mpango, ameagiza kukamilika haraka kwa ujenzi wa kituo cha afya cha Kabuku, ili kuendeleza jitihada za Serikali ya Rais Mhe Dk Samia Suluhu Hassan, kuboresha afya za wananchi wake.

Naye Meneja wa TANESCO katika wilaya ya Handeni, Mwalimu Mussa Kassim, baada ya kuruhusiwa na Mhe Dk Mpango, akasema vijini 91 na mitaa 60 iliyopo wilayani humo imefikiwa na huduma ya umeme na kwamba vitongoji 250 kati ya 770 vilivyopo halmashauri ya wilaya hiyo ndivyo havijafikiwa na miundombinu ya umeme.

Mwalimu Kassim amemhakikishia Mhe Dk Mipango kuwa vitongoji hivyo vitafikiwa na huduma hiyo kabla ya Uchaguzi Mkuu wa 2025.

Matangazo

  • TANGA REGION INVESTMENT GUIDE November 24, 2023
  • SENSA YA WATU NA MAKAZI MWAKA 2022 MKOA WA TANGA June 13, 2023
  • Angalia zote

Habari mpya

  • AWESO AKABIDHI VIFAA VYA MRADI WA MAJI MKINGA-HOROHORO

    January 17, 2026
  • VIJANA PANGANI 'WAKOSHWA' NA MIKOPO YA ASILIMIA 10

    November 27, 2025
  • BOMBO YAZINDUA WODI BINAFSI KUBORESHA HUDUMA ZA AFYA TANGA

    November 27, 2025
  • EACOP YAELEZA MAENDELEO YA MRADI WA BOMBA LA MAFUTA GHAFI

    November 25, 2025
  • Angalia zote

Video

KATIBU TAWALA MKOA WA TANGA AKIONGOZA WATUMISHI WA MKOA HUO KUFANYA MAZOEZI YA PAMOJA KATIKA UWANJA WA MKWAKWANI KUITIKIA WITO WA MHE. MAKAMU WA RAIS
Video zaidi

Viunganishi vya haraka

Tovuti zinazoendana

  • TAMISEMI
  • Kupata huduma za kiutumishi
  • Wakala ya Serikali Mtandao
  • Utumishi
  • Baraza la Mitihani Tanzania (NECTA)
  • Tovuti ya Serikali

Kifuatilia watazamaji duniani

world map hits counter

idadi ya watazamaji

free HitCounter

Ramani ya Mkoa wa Tanga

Wasiliana nasi

    Golf Area/Masiwani Road Tanga

    Anuani ya posta: P.O.Box 5095 Tanga

    Simu: 027 2642421

    Simu ya Mkononi:

    Barua pepe: ras.tanga@tamisemi.go.tz

Anuani zingine

   

    • Sera za faragha
    • Kanusho
    • Maswali na Majibu
    • Ramani ya Tovuti
    • Huduma

Haki miliki ©2017 Katibu Tawala Mkoa wa Tanga . Haki zote zimehifadhiwa.