Na Mashaka Mgeta, OMM TANGA
MKUU wa Mkoa wa Tanga, Mhe Balozi Dkt Batlida, ameiasa jamii kujenga tabia ya kusaidia hususani kwenye kipindi hiki cha mfungo wa Ramadhani na Kwaresma, kwani ni sehemu ya ibada katika kusaidia wenye uhitaji.
Mhe Balozi Dkt Batilda, ameyasema hayo kwenye hafla ya kukabidhi vyereheni kwa watu wenye wenye mahitaji maalum, vilivyotolewa na wanawake wa Jumuiya ya Bohora mkoani Tanga.
"Niwashukuru wanawake wa Jumuiya ya Bohora kwa kusaidiana na Serikali katika kuwashika mkono wenye uhitaji maalum, jambo ambalo linaleta baraka na mwanzo mpya wa kujijenga kiuchumi kwa walengwa hao,"alisema Mhe Balozi Dkt Batilda.
Wanawake hao wa Bohora, wametoa msaada wa vyerehani kuwasaidia wenye mahitaji maalum kujipatia kipato kupitia ushonaji nguo.
Vyerehani hivyo vimekabidhiwa kwa wahitaji, mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Mhe Balozi Dkt Batlida Buriani ofisini kwake Machi 29, 2025.
Wanawake hao wamesema msaada huo ni sehemu ya sadaka wanazozitoa kila mwaka kusaidia makundi yenye uhitaji.
Akiongea kwa niaba ya wenzake, Fatema Mamujee, alisema mwaka huu wameguswa kutoa msaada wa vyerehani kwa wanawake wenye mahitaji maalum jijini Tanga, wakiwalenga wenye ujuzi wa kushona nguo.
"Msaada huo utasaidia pia familia zao na kuwainua kiuchumi kupitia fursa ya ufundi nguo, na hivyo kuimarisha hali zao za kiuchumi, "alisema Mamujee.
Golf Area/Masiwani Road Tanga
Anuani ya posta: P.O.Box 5095 Tanga
Simu: 027 2642421
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ras.tanga@tamisemi.go.tz
Haki miliki ©2017 Katibu Tawala Mkoa wa Tanga . Haki zote zimehifadhiwa.