• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali na Majibu |
    • Barua pepe |
Tanga Region
Tanga Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Tanga

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Dira na Dhima
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za maji
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
    • Idara
      • Utawala na Utumishi
      • Mipango na Uratibu
      • Miundombinu
      • Elimu
      • Afya
      • Maji
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Usimamizi wa Serikali za Mitaa
    • Vitengo
      • TEHAMA
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa ndani
      • Manunuzi
      • Sheria
  • Machapisho
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu za Maombi
    • Hotuba
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Sehemu ya picha
    • Habari
    • Matukio
  • Miradi
    • Miradi iliyokamilika
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya Pangani
    • Halmashauri ya Wilaya Mkinga
    • Halmashauri ya Wilaya Muheza
    • Halmashauri ya Jiji Tanga
    • Halmashauri ya Wilaya Korogwe
    • Halmashauri ya Mji Korogwe
    • Halmashauri ya Wilaya Handeni
    • Halmashauri ya Mji Handeni
    • Halmashauri ya Wilaya Kilindi
    • Halmashauri ya Wilaya Lushoto

MADAKTARI NA TUNU ZA UADILIFU KATIKA UTOAJI HUDUMA BORA KWA JAMII

Imewekwa tarehe: June 16th, 2025

Na Mashaka Mgeta, OMM TANGA

MADAKTARI mkoani Tanga, wametakiwa kuenzi na kuzitumia tunu za uadilifu katika utoaji huduma kwa wananchi, ili kufikia lengo la kuwaponya na kuleta nafuu kwa wahitaji.

Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru 2025, Ismail Ali Ussi, ametoa rai hiyo alipozungumza katika hafla ya kuweka jiwe la msingi kwenye mradi wa ujenzi wa jengo la mionzi la Kituo cha Afya Makorora jijini Tanga.

Mwenge wa Uhuru wenye ujumbe unaosema JITOKEZE KUSHIRIKI UCHAGUZI MKUU WA 2025 KWA AMANI NA UTULIVU, unakimbizwa kwenye Halmashauri ya Jiji la Tanga utakapotembelea, kukagua, kuweka jiwe la msingi ama kufungua jumla ya miradi saba ya kisekta.

Ussi amesema, uboreshaji wa sekta ya afya, kama ilivyo kwenye sekta nyingine kunakosafanywa na Serikali ya Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan, kunachochea pia uwepo wa mazingira bora kwa watumishi wa umma.

”Kunapokuwa na mazingira magumu kwenye hospitali zetu, hata madaktari hawafanyi kazi zao ipasavyo, hivyo tunapopata jengo la huduma za mionzi kama hili, ni wazi kwamba madaktari wetu wanakwenda kuboresha zaidi utendaji kazi wao,” anasema.

Mradi huo uliohusisha vyumba viwili vya kupiga mionzi (X-ray) na ultrasound, unagharimu Shilingi milioni 84.7 za mapato ya ndani, unatekelezwa kupitia fedha za mapato ya ndani ya Kituo hicho.

Mradi huo wenye gharama ya Shilingi milioni 84.7 ulianza Oktoba 21, mwaka jana  na kukamilika Aprili 24 mwaka huu, ukiwa umetumia njia ya “Force account” na mfumo wa manunuzi kwa njia ya NeST.

Matangazo

  • TANGA REGION INVESTMENT GUIDE November 24, 2023
  • SENSA YA WATU NA MAKAZI MWAKA 2022 MKOA WA TANGA June 13, 2023
  • Angalia zote

Habari mpya

  • RAS MCHATTA: SINA MANENO MENGI, NIPIMENI KWA KAZI, UWAJIBIKAJI

    June 30, 2025
  • BALOZI BATILDA AAGIZA WAKUU WA WILAYA KUSIKILIZA KERO, AWAAPISHI WAWILI TANGA

    June 30, 2025
  • RC BATILDA ATAKA MAADILI, UTAWALA BORA KUIMARISHWA SERIKALINI

    June 25, 2025
  • MIAKA MINNE, SIKU 23 ZA RAS MNYEMA TANGA, AHAMISHIWA PWANI

    June 24, 2025
  • Angalia zote

Video

KATIBU TAWALA MKOA WA TANGA AKIONGOZA WATUMISHI WA MKOA HUO KUFANYA MAZOEZI YA PAMOJA KATIKA UWANJA WA MKWAKWANI KUITIKIA WITO WA MHE. MAKAMU WA RAIS
Video zaidi

Viunganishi vya haraka

Tovuti zinazoendana

  • TAMISEMI
  • Kupata huduma za kiutumishi
  • Wakala ya Serikali Mtandao
  • Utumishi
  • Baraza la Mitihani Tanzania (NECTA)
  • Tovuti ya Serikali

Kifuatilia watazamaji duniani

world map hits counter

idadi ya watazamaji

free HitCounter

Ramani ya Mkoa wa Tanga

Wasiliana nasi

    Golf Area/Masiwani Road Tanga

    Anuani ya posta: P.O.Box 5095 Tanga

    Simu: 027 2642421

    Simu ya Mkononi:

    Barua pepe: ras.tanga@tamisemi.go.tz

Anuani zingine

   

    • Sera za faragha
    • Kanusho
    • Maswali na Majibu
    • Ramani ya Tovuti
    • Huduma

Haki miliki ©2017 Katibu Tawala Mkoa wa Tanga . Haki zote zimehifadhiwa.