• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali na Majibu |
    • Barua pepe |
Tanga Region
Tanga Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Tanga

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Dira na Dhima
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za maji
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
    • Idara
      • Utawala na Utumishi
      • Mipango na Uratibu
      • Miundombinu
      • Elimu
      • Afya
      • Maji
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Usimamizi wa Serikali za Mitaa
    • Vitengo
      • TEHAMA
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa ndani
      • Manunuzi
      • Sheria
  • Machapisho
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu za Maombi
    • Hotuba
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Sehemu ya picha
    • Habari
    • Matukio
  • Miradi
    • Miradi iliyokamilika
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya Pangani
    • Halmashauri ya Wilaya Mkinga
    • Halmashauri ya Wilaya Muheza
    • Halmashauri ya Jiji Tanga
    • Halmashauri ya Wilaya Korogwe
    • Halmashauri ya Mji Korogwe
    • Halmashauri ya Wilaya Handeni
    • Halmashauri ya Mji Handeni
    • Halmashauri ya Wilaya Kilindi
    • Halmashauri ya Wilaya Lushoto

MGUMBA ATEMBELEA VIWANDA

Imewekwa tarehe: February 23rd, 2023

Na Emma Kigombe

Serikali Mkoani Tanga imeendelea kuweka mazingira rafiki kwa wawekezaji hasa wa viwanda ili kuirudisha Tanga ya zamani ya viwanda na kuweka mazingira rafiki kwa wawekezaji wengine

Hayo yamebainishwa na Mkuu wa Mkoa wa Tanga Mhe. Omary Mgumba katika ziara yake ya kutembelea viwanda mbalimbali mkoani humo ikiwa ni jitihada za kufuatilia utekelezaji wa maelekezo ya Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ya kuirudisha Tanga kwenye hadhi yake ya viwanda.

Akizungumza mara baada ya kutembelea kiwanda cha kadi Mkuu wa Mkoa wa Tanga Omary Mgumba amesema kuwa Mkoa umeweka mazingira rafiki kwa wawekezaji wote ili kupata matokeo mazuri na kuwapa fursa wawekezaji kuwekeza zaidi.

" Tumeweka mazingira mazuri kwa ajili ya kuvutia wawekezaji na moja ya matokeo hayo ndio uwekezaji huu unaofanywa na kiwanda hiki cha pekee Afrika Mashariki ambapo kwa Afrika vipo viwanda viwili kimoja kipo Tanzania Mkoani Tanga na kingine Afrika kusini" alisema Mgumba

Aidha Mgumba ametoa pongezi kwa mwekezaji kwa kuichagua Tanga kufungua kiwanda hicho cha pekee ambacho kina manufaa makubwa kwa wananchi wa mkoa wa Tanga na Taifa kwa ujumla.

Pia Mgumba amesema ameridhishwa na maendeleo ya kiwanda cha uzalishaji kadi za kielektroniki ( smart card) kwa kuwa katika hatua za mwisho kuanza uzalishaji.

"Kama tulivyoshuhudia ,wapo katika hatua za mwisho ya majaribio za kutengeneza kadi za kimtandao kwa hiyo uwepo wa kiwanda hiki ni moja ya jitihada za Mhe. Rais Rais katika ujenzi wa viwanda na kutengeneza ajira kwa watanzania" aliongeza Mgumba

Sambamba na hilo Mkuu wa Mkoa wa Tanga Mhe Omary Mgumba akatoa wito kwa wadau mbalimbali kuunga mkono jitihada za Mhe Rais katika kununua bidhaa zinazozalishwa kwenye viwanda hivyo.

"Nitoe wito kwa wadau wote ambao wanategemea kazi kwa ajili ya kazi zao kuja Tanga na kuonana na kiwanda hiki kuwapa tenda badala ya kupeleka nje ya nchi wazitengeneze kadi hizo hapa Tanzania kwa ajili ya kuokoa uchumi wetu na kutengeneza ajira nyingi kwa watanzania" alisema Mgumba

Kwa upande wake Mstahiki Meya wa Jiji la Tanga Abdurahman Shiloow amesema uwepo wa viwanda hivyo ndani ya Jiji na Mkoa wa Tanga vitasaidia kuwanufaisha wananchi katika suala zima la kupata ajira na kuiongezea serikali mapato kupitia kodi zinazolipwa na wawekezaji hao.

Nae mmiliki wa kiwanda cha kadi na vocha Rashid Liemba amesema kiwanda hicho kitakapo anza kufanya kazi kitatoa ajira kwa wananchi wa Tanga huku kikileta fedha nyingi za kigeni

" Biashara kubwa tunayoifanya tunapeleka fedha zetu nchi za nje kununua kadi lakini sasa hivi tunatengeneza kwenye nchi yetu mtusaidie katangaza soko lilipo" Alisema Liemba.

Katika hatua nyingine Mkuu wa mkoa Omary Mgumba ametembelea kiwanda cha vipodozi cha Ashers ambapo mara baada ya kupitishwa katika maeneo mbalimbali ya uzalishaji wa kiwanda hicho alisema kuwa amefurahishwa na kiwanda hicho kuwa ni miongoni mwa walipa kodi wazuri katika mkoa wa Tanga

"Kwa taarifa na takwimu nilizokuwa nazo kiwanda hiki kimekuwa kikilipa kodi vizuri na kwa wakati na kiasi ambacho tunakubaliana" alisema Mgumba

Aidha Mgumba alisema jambo kubwa alilovutiwa nalo katika ziara yake kiwandani hapo ambalo linatupa funzo sisi watanzania ni kuendeleza urithi ambao tumeachiwa na waazilishi wetu kwa kuwa kiwanda hicho mpaka sasa ni kizazi cha tatu na bado kinaendelea kufanya vizuri katika uzalishaji.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa kiwanda cha vipodozi  Ashers Vanden Ashers ameishukuru serikali ya Mkoa wa Tanga kufika kiwandani hapo na kuchukua changamoto ambapo anaamini ujio huo utaenda kuleta mapinduzi makubwa kwenye sekta ya viwanda Mkoani humo.

Dhamira ya Serikali ni kuhakikisha Mkoa wa Tanga unarudi kwenye hadhi yake ya viwanda kwa kuwawekea mazingira rafiki wawekezaji wote mkoani humo.

Matangazo

  • TANGA REGION INVESTMENT GUIDE November 24, 2023
  • SENSA YA WATU NA MAKAZI MWAKA 2022 MKOA WA TANGA June 13, 2023
  • Angalia zote

Habari mpya

  • RAS MCHATTA: SINA MANENO MENGI, NIPIMENI KWA KAZI, UWAJIBIKAJI

    June 30, 2025
  • BALOZI BATILDA AAGIZA WAKUU WA WILAYA KUSIKILIZA KERO, AWAAPISHI WAWILI TANGA

    June 30, 2025
  • RC BATILDA ATAKA MAADILI, UTAWALA BORA KUIMARISHWA SERIKALINI

    June 25, 2025
  • MIAKA MINNE, SIKU 23 ZA RAS MNYEMA TANGA, AHAMISHIWA PWANI

    June 24, 2025
  • Angalia zote

Video

KATIBU TAWALA MKOA WA TANGA AKIONGOZA WATUMISHI WA MKOA HUO KUFANYA MAZOEZI YA PAMOJA KATIKA UWANJA WA MKWAKWANI KUITIKIA WITO WA MHE. MAKAMU WA RAIS
Video zaidi

Viunganishi vya haraka

Tovuti zinazoendana

  • TAMISEMI
  • Kupata huduma za kiutumishi
  • Wakala ya Serikali Mtandao
  • Utumishi
  • Baraza la Mitihani Tanzania (NECTA)
  • Tovuti ya Serikali

Kifuatilia watazamaji duniani

world map hits counter

idadi ya watazamaji

free HitCounter

Ramani ya Mkoa wa Tanga

Wasiliana nasi

    Golf Area/Masiwani Road Tanga

    Anuani ya posta: P.O.Box 5095 Tanga

    Simu: 027 2642421

    Simu ya Mkononi:

    Barua pepe: ras.tanga@tamisemi.go.tz

Anuani zingine

   

    • Sera za faragha
    • Kanusho
    • Maswali na Majibu
    • Ramani ya Tovuti
    • Huduma

Haki miliki ©2017 Katibu Tawala Mkoa wa Tanga . Haki zote zimehifadhiwa.