Na Emma Kigombe
Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Mhe.Omary Mgumba amekitaka Chama cha Walimu Tanzania (CWT), kuendeleza umoja na mshikamano na kuepuka mifarakano kwa maslahi mapana ya chama hicho na walimu kwa ujumla.
Akizungumza wakati akifungua kikao cha chama hicho kilichofanyika mkoani Tanga na kujumuisha wajumbe kutoka mikoa yote nchini, Mgumba amesema kupitia salam zao basi ni vema wakaziishi ili kudumisha umoja na mshikamano ndani ya chama ili kufikia malengo waliyojiwekea.
"Muendeleze utulivu mshikamano na umoja ndani ya chama chenu na umoja wenu kwa walimu salamu yenu hii muiishi hasa ile ya mshikamano salamu zenu zote ni nzuri ila mimi nimevutiwa na ile ukimchokoza mwalimu mmoja umewachokoza wote kwa sababu jambo la walimu ni jambo la walimu wote hivyo tuendeleze ushirikiano sababu bila kuwa na umoja hata malengo yenu hamtayafikia," alisema Mgumba.
Aidha Mgumba amesema serikali itaendelea kutoa ushirikiano siku zote kwa kuwa inatambua umuhimu wa walimu kwa Taifa.
Aidha Mgumba amemuagiza Afiisa Tawala msaidizi upande wa elimu kuhakikisha shule za binafsi zinafuata sheria na taratibu zilizowekwa katika kuhakikisha mwanafunzi anasoma bila usumbufu wowote wa kurudishwa nyumbani sababu ya ada ama mchango wowote badala yake uongozi uwasiliane na mzazi ili kutatua changamoto hizo.
" Shule za binafsi ni kweli zina malengo katika biashara na faida lakini serikali imetoa maelekezo mazuri juu ya suala hili lakini wenzetu wa shule binafsi mtoto kama hajalipa ada au mchango wowote adhabu ya kwanza ni kumrudisha mtoto nyumbani, huu ni ukiukwaji wa maelekezo ya serikali kama kuna mtoto hajalipa ada mtoto aendelee na masomo yake asibugudhiwe wamiliki wa shule na walimu wa shule hizo wawasiliane na mzazi wa huyo mtoto Mgumb.
Aidha, Mgumba amewaomba wazazi wanaoshindwa kuwalipia ada na michango mingine watoto wao wakafanya maamuzi ya kuwahamishia watoto katika shule za serikali kwa kuwa imewekeza fedha nyingi kwenye uboreshaji wa miundombinu ya elimu kwa manufaa ya Watanzania wote.
"Kwa wazazi na walezi, Dkt. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania amejenga shule za kutosha ameondoa ada zote elimu bila malipo lengo kuwawezesha Watanzania wote watoto wao wapate elimu kwa urahisi" aliongeza Mgumba.
Katika hatua nyingine, Mhe. Mgumba amewataka walimu kuendelea kufundisha elimu ya taaluma na ujuzi bila kusahau elimu ya malezi na maadili kwa watoto kwa sababu mtoto muda mwingi anakaa na mwalimu kuliko mzazi hivyo wasaidie kuwarudisha watoto kwenye maadili mema kwa kuzingatia mila na desturi za Kitanzania.
Mhe. Mgumba pia amewakumbusha walimu kusimamia maadili na kupinga vita vitendo vya ukatili kwa watoto kwa kuwa nao karibu na kuwapa elimu juu ya suala hilo.
ReplyForward |
Golf Area/Masiwani Road Tanga
Anuani ya posta: P.O.Box 5095 Tanga
Simu: 027 2642421
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ras.tanga@tamisemi.go.tz
Haki miliki ©2017 Katibu Tawala Mkoa wa Tanga . Haki zote zimehifadhiwa.