• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali na Majibu |
    • Barua pepe |
Tanga Region
Tanga Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Tanga

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Dira na Dhima
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za maji
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
    • Idara
      • Utawala na Utumishi
      • Mipango na Uratibu
      • Miundombinu
      • Elimu
      • Afya
      • Maji
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Usimamizi wa Serikali za Mitaa
    • Vitengo
      • TEHAMA
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa ndani
      • Manunuzi
      • Sheria
  • Machapisho
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu za Maombi
    • Hotuba
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Sehemu ya picha
    • Habari
    • Matukio
  • Miradi
    • Miradi iliyokamilika
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya Pangani
    • Halmashauri ya Wilaya Mkinga
    • Halmashauri ya Wilaya Muheza
    • Halmashauri ya Jiji Tanga
    • Halmashauri ya Wilaya Korogwe
    • Halmashauri ya Mji Korogwe
    • Halmashauri ya Wilaya Handeni
    • Halmashauri ya Mji Handeni
    • Halmashauri ya Wilaya Kilindi
    • Halmashauri ya Wilaya Lushoto

MWENGE KUFUATILIA MILIONI 478 ZA KUMALIZIA MRADI WA MAJI HANDENI

Imewekwa tarehe: April 21st, 2024

MWENGE KUFUATILIA MILIONI 478 ZA KUMALIZIA MRADI WA MAJI HANDENI

Na Mashaka Mgeta, HANDENI

MWENGE wa Uhuru Kitaifa 2024, umeingilia kati na kuomba barua ya kukumbushia na kufuatilia Shilingi milioni 400 za kumalizia mradi wa maji Kwenkambala, uliopo wilaya ya Handeni mkoani Tanga.

Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa 2024, Godfrey Mnzava, amemuelekeza Mkuu wa Wilaya ya Handeni, Mhe Albert Msando, kumpatia nakala ya barua ya kukumbushia malipo hayo, ili Mwenge wa Uhuru uwasiliane na Waziri wa Maji, Mhe Jumaa Aweso, kwa ajili ya kuongeza nguvu ya fedha hizo kutolewa zitumike kwa umaliziaji wake.

Mnzava, ametoa agizo hilo wakati Mwenge wa Uhuru 2024 ulipotembelea mradi wa  Kwenkamba unaotekelezwa na Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira (HTM) kwa kutumia wataalam wa ndani (Force Account).

Mkurugenzi Mtendaji wa HTM, Mhandisi Yohana Mgaza amesema, utekelezaji wa mradi huo umefikia asilimia 70 na ili kukamilika kwake, zinahitajika Shilingi 478,693,408.20 kwa ajili ya ununuzi na ulazaji wa mabomba, ujenzi wa vituo, ujenzi wa chemba pamoja na gharama za usimamizi.

Amesema Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira (RUWASA) imeandika barua Wizara ya Maji kukumbushia kupewa kiasi hicho cha fedha, kauli iliyomfanya Mnzava, kuhitaji nakala ya barua hiyo kwa ufuatiliaji.

Mhandishi Mgaza amesema, lengo la mradi huo ni kutoa huduma ya majisafi na salama kwa wananchi wa kata ya Kwediyamba wapatao 5,746.

Amesema mradi huo ulioanza kutekelezwa Septemba 11, 20222, ulitegemewa kukamilka Septemba 10, 2023, lakini kutokana na fedha kutopatikana kwa wakati, haujakamilika hadi sasa na kwamba unatarajiwa kukamilika Juni 2024,.

Mhandisi Mgaza amesema mradi huo utagharimu Shilingi takribani bilioni 1.3 kutoka Serikali Kuu na kwamba hadi kufikia leo Aprili 19, 2024, HTM imepokea Shilingi milioni 800 kwa awamu tatu kuanzia mwaka 2022/23 na 2023/24.

Kwa mujibu wa Mhandisi Mgaza, zazi zilizopangwa kutekelezwa ni pamoja na ufungaji wa pampu ya kusukumia maji, kuchimba mtaro na kulaza bomba kuu la kipenyo cha milimita 110 (PN16 & PN10) umbali wa mita 5,925 na ujenzi wa tenki la kuhifadhia maji lenye uwezo wa kuhifadhi lita 150,000 kwenye Mnara wa mita 9 katika mtaa wa Mpakani.

Kazi nyingine ni kuchimba mtaro na kulaza mtandao wa mabomba ya kusambaza maji ya vipenyo kuanzia milimita 32 hadi 160 (PN 12.5 & PN10) kwa umbali wa mita 17,920, ujenzi wa vituo/vilula 29 vya kuchotea maji.

Aidha, Mhandisi Mgaza amesema wananchi wa eneo hilo wamechangia mradi kwa kutoa maeneo yao bure yenye ukubwa wa zaidi ya ½ ekari, yenye thamani ya Shilingi 5,000,000 kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu ya mradi.

Amesema jumla ya Shilingi milioni 800 zimetumika kutekeleza shughuli  za usanifu wa mradi na maandalizi ya michoro, ujenzi wa tenki lenye ujazo wa lita 150,000 kwenye mnara wa mita tisa, kuchimba mtaro na kulaza bomba kuu la kipenyo cha milimita 110 (PN16, PN 12.5 na PN10) umbali wa mita 5,925.

Shughuli nyingie ni kuchimba mtaro na kulaza bomba kuu la kusambazia maji kipenyo cha milimita 150 (PN 12 na PN10) umbali wa mita 2,000 na kuchimba mtaro na kulaza bomba la kusambaza maji lenye kipenyo cha milimita 63, milimita 50, na milimita 32 (PN10) umbali wa mita 1,650.

Matangazo

  • MATOKEO YA MTIHANI WA KIDATO CHA NNE (CSEE)2023 January 25, 2024
  • HOTUBA YA MKUU WA MKOA WA TANGA MHE. WAZIRI WAZIRI KINDAMBA KATIKA HAFLA YA UFUNGUZI WA KONGAMANO LA UWEKEZAJI NA UZINDUZI WA MWONGOZO WA FURSA ZA UWEKEZAJI MKOA WA TANGA 16/11/2023 November 27, 2023
  • FORM ONE SELECTION 2024 December 20, 2023
  • TANGA REGION INVESTMENT GUIDE November 24, 2023
  • Angalia zote

Habari mpya

  • SAFARI YA RAIS SAMIA KWA SGR YAIBUA HISIA ZA WAKAZI WA TANGA

    May 17, 2025
  • CCM TANGA YATETA SAFARI ZA RAIS SAMIA NJE YA NCHI

    May 16, 2025
  • DC LUSHOTO ASEMA NIDHAMU, UADILIFU NI NYENZO ZA UFANISI MIRADI YA PEMBEZONI

    May 16, 2025
  • CCM: TUSIWE 'WANYAMPALA' KATIKA KUKAGUA MIRADI YA MAENDELEO

    May 16, 2025
  • Angalia zote

Video

KATIBU TAWALA MKOA WA TANGA AKIONGOZA WATUMISHI WA MKOA HUO KUFANYA MAZOEZI YA PAMOJA KATIKA UWANJA WA MKWAKWANI KUITIKIA WITO WA MHE. MAKAMU WA RAIS
Video zaidi

Viunganishi vya haraka

Tovuti zinazoendana

  • TAMISEMI
  • Kupata huduma za kiutumishi
  • Wakala ya Serikali Mtandao
  • Utumishi
  • Baraza la Mitihani Tanzania (NECTA)
  • Tovuti ya Serikali

Kifuatilia watazamaji duniani

world map hits counter

idadi ya watazamaji

free HitCounter

Ramani ya Mkoa wa Tanga

Wasiliana nasi

    Golf Area/Masiwani Road Tanga

    Anuani ya posta: P.O.Box 5095 Tanga

    Simu: 027 2642421

    Simu ya Mkononi:

    Barua pepe: ras.tanga@tamisemi.go.tz

Anuani zingine

   

    • Sera za faragha
    • Kanusho
    • Maswali na Majibu
    • Ramani ya Tovuti
    • Huduma

Haki miliki ©2017 Katibu Tawala Mkoa wa Tanga . Haki zote zimehifadhiwa.