MWENGE WAELEKEZA KUDHIBITI UVAMIZI MAENEO YA UMMA
Na Mashaka Mgeta, MUHEZA
MWENGE wa Uhuru 2025 umezielekeza Mamlaka za Serikali za Mitaa (LGAs) kuweka na kutekeleza mipango inayolenga kudhibiti vitendo vya uvamizi wa maeneo ya umma.
Kiongozi wa Mwenge wa Uhuru 2025, Ismail Ali Ussi, ametoa rai hiyo alipokuwa akizungumza na wakazi wa Halmashauri ya Wilaya ya Muheza, kwenye mradi ujenzi ya Zahanati ya Kijiji cha Muungano uliopo kata ya Mlingano, uliotembelewa, kukaguliwa na kuwekewa jiwe la msingi.
Mradi huo wenye lengo la kuwezesha upatikanaji wa huduma bora za afya, kusogeza huduma za mama,baba na mtoto karibu na wananchi na hivyo kuwafanya watu kuwa wenye afya njema, unagharimu Shilingi milioni 165.9 huku walengwa wake wakiwa ni wakazi 6,258 wa kijiji cha Muungano.
Amesema kuna kasumba kwa baadhi ya maeneo ya umma na yaliyopangiwa huduma za kijamii, kuvamiwa na watu wasiokuwa na nia njema, kisha wakaachwa na kufanya maendelezo, hali inayoibua taharuki pindi wanapoondolewa.
Ussi amesema, Serikali imekuwa na mipango ya muda mfupi, kati na mrefu wa uendelezaji wa maeneo kwa shughuli za kijamii, hivyo ni muhimu kwa mamlaka za usimamizi kudhibiti aina zote za uvamizi usitokee kwenye maeneo yao
Hata hivyo,vyo, Ussi amesema watu wanaoshiriki uvamizi wa maeneo ya Serikali na yale ya umma, wanapaswa kuepuka vitendo hivyo kwani ni kinyume cha sheria zilizopo.
Mganga Mkuu wa Wilaya ya Muheza, Dk Fani Musa akasema mradi huo unaofadhiliwa na taasisi ya Islamic Help, ukiwa umekamilika kwa asilimia 90. ulianza Machi,2, mwaka huu na unatarajiwa kukamilika Agosti, 1, 2025.
Golf Area/Masiwani Road Tanga
Anuani ya posta: P.O.Box 5095 Tanga
Simu: 027 2642421
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ras.tanga@tamisemi.go.tz
Haki miliki ©2017 Katibu Tawala Mkoa wa Tanga . Haki zote zimehifadhiwa.