Na Emma Kigombe, OMM TANGA
WAZIRI Mkuu Mstaafu, Mhe Mizengo Kayanza Pinda, amehimiza ushirikiano endelevu kati ya Serikali na jamii katika kusukuma mbele ajenda za maendeleo.
Mhe Pinda ameyasema hayo leo Julai 9, 2025 alipomtembelea Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Mhe Balozi Dkt Batilda Burian ofisini kwake jijini Tanga.
Viongozi wengine waliohudhiria kikao hicho ni pamoja na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Tanga, Rajab Abdallah na Katibu Tawala Mkoa, Rashid Mchatta.
Mhe Pinda, amewapongeza viongozi wa mkoa huo kwa juhudi za kuboresha maisha ya wananchi kupitia utekelezaji na usimamizi wa miradi mbalimbali ya maendeleo.
Kupitia kikao hicho, viongozi hao walibadilishana mawazo na uzoefu kuhusu masuala tofauti yanayohusu maendeleo na ustawi wa wakazi wa Tanga, hususan katika sekta za kilimo, afya, elimu na viwanda.
Kwa upande wake, Mhe Balozi Dkt Batilda, amemshukuru Mhe Pinda kwa ziara ya kirafiki na maendeleo, huku akimweleza mafanikio mbalimbali yaliyopatikana katika maeneo tofauti ya kisekta.
Golf Area/Masiwani Road Tanga
Anuani ya posta: P.O.Box 5095 Tanga
Simu: 027 2642421
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ras.tanga@tamisemi.go.tz
Haki miliki ©2017 Katibu Tawala Mkoa wa Tanga . Haki zote zimehifadhiwa.