Na Mashaka Mgeta, OMM TANGA
MAZINGIRA bora ya biashara yanayochochewa na mahusiano mema ya Serikali ya Mhe Rais Dkt Samia Suluhu Hassan, yanaendelea kukuza biashara, mitaji na uwekezaji, hivyo kuzalisha faida inayorejeshwa kwa umma.
Kampuni ya Saruji Tanga, ni miongoni mwa taasisi zinazonufaika kwa mazingira bora hayo, hivyo kushawishika kuunga mkono jitihada za kuwawezesha wanawake na vijana mkoani Tanga.
Mwenyekiti wa kampuni hiyo, Hakan Gordal, leo Julai 3, 2025, amemkabidhi Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Mhe Balozi Dkt Batilda Burian, bajaji 10 za kisasa zinazotumia umeme badala ya mafuta, zenye thamani ya jumla ya Shilingi milioni milioni 65.
Amesema bajaji za umeme ni sehemu ya uthibitisho wa utekelezaji wa sera za kampuni katika utunzani mazingira na kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi yanayochangiwa na uchafuzi wa hewa.
Gordal, hatua ya kutoa bajaji hizo inazotokana na mawasiliano yao na Mhe Balozi Dkt Batilda, aliyeainisha mahitaji ya vyombo vya usafiri wa kibiashara hususani kwa wanawake na vijana wa makundi maalum.
Amesema Tanga ni eneo la kimkakati kwa biashara yao inayotarajiwa kuzalisha saruji itakayouzwa nje ya nchi katika siku chache zijazo.
Kwa mujibu wa Goldal, ufanisi na mafanikio ya kampuni hiyo vinachangiwa kwa kiasi kikubwa na mahusiano mema kati yao (wawekezaji), Serikali na wakazi wa mkoa wa Tanga kunapofanyika shughuli za uzalishaji wa saruji.
Naye Mhe Balozi Dkt Batilda, amesema imekuwa ’safari ndefu’ ya mazungumzo na uongozi wa kampuni hiyo, hasa baada ya kuwepo hisia za kufungwa kwa uzalishaji, kutokana na kununuliwa na kampuni ya Saruji Twiga.
Amesema, ushuhuda uliopo Tanga unathibitisha kuwepo wawekezaji walionunua viwanda vya awali, kutoviendeleza na wengine kung’oa mitando na kuihamishia mikoa kama vile Arusha na Dar es Salaam.
Mhe Balozi Dkt Batilda amesema, kwa hali hiyo, kampuni ya Saruji Tanga inakuwa miongoni mwa wadau wakubwa wanaotekeleza dhamira ya Mhe Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kuurejesha mkoa huo kuwa wa viwanda.
Amesema uzalishaji na biashara ya kiwanda hicho, utaendeleza ukuzaji wa pato la mkoa huo na Taifa, huku kukiwa na ustawishaji wa maisha ya watu kupitia ajira zilizo na zisizokuwa za moja kwa moja.
Mhe Balozi Dkt Batilda amesema, miongoni mwa wanufaika wa awali wa bajaji hizo ni wasichana watatu wanaoendesha bodaboda na wanaoishi na ulemavu wawili.
Amesema wanufaika hao na wengine, wataingia mkataba wa marejesho utakaowezesha kupata fedha za kuagiza bajaji nyingine ili kuongeza idadi ya wanufaika.
Golf Area/Masiwani Road Tanga
Anuani ya posta: P.O.Box 5095 Tanga
Simu: 027 2642421
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ras.tanga@tamisemi.go.tz
Haki miliki ©2017 Katibu Tawala Mkoa wa Tanga . Haki zote zimehifadhiwa.