• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali na Majibu |
    • Barua pepe |
Tanga Region
Tanga Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Tanga

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Dira na Dhima
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za maji
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
    • Idara
      • Utawala na Utumishi
      • Mipango na Uratibu
      • Miundombinu
      • Elimu
      • Afya
      • Maji
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Usimamizi wa Serikali za Mitaa
    • Vitengo
      • TEHAMA
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa ndani
      • Manunuzi
      • Sheria
  • Machapisho
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu za Maombi
    • Hotuba
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Sehemu ya picha
    • Habari
    • Matukio
  • Miradi
    • Miradi iliyokamilika
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya Pangani
    • Halmashauri ya Wilaya Mkinga
    • Halmashauri ya Wilaya Muheza
    • Halmashauri ya Jiji Tanga
    • Halmashauri ya Wilaya Korogwe
    • Halmashauri ya Mji Korogwe
    • Halmashauri ya Wilaya Handeni
    • Halmashauri ya Mji Handeni
    • Halmashauri ya Wilaya Kilindi
    • Halmashauri ya Wilaya Lushoto

RAIS SAMIA 'AWALILIA' 11 WALIOFARIKI AJALI YA GARI HANDENI

Imewekwa tarehe: January 14th, 2025

Na Mashaka Mgeta, HANDENI

SIMANZI, majonzi na vilio vimetanda kuanzia usiku wa jana Januari 13,2025, kwenye kata ya Segera, wilaya ya Handeni mkoani Tanga, kufuatia vifo vya watu 11 na majeruhi 13, kutokana na ajali ya gari.

Mhe Rais Dk Samia Suluhu Hassan, ametuma salaam za rambirambi kufuatia vifo hivyo, kutoa pole na kuwatakia kupona haraka majeruhi wa ajali hiyo

Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Mhe Balozi Dk Batilda Burian, pamoja na kuwasilisha salaam za Mhe Rais Dk Samia, amesema ajali hiyo imesababishwa na roli la mizigo lenye namba T 782 BTU.

Amesema, roli hilo liliacha barabara na kuelekea mahali walipokuwa watu wakiwaokoa majeruhi kutoka kwenye gari nyingine iliyotokea awali, ikilihusisha gari aina ya Tata lenye namba T 720 EJP.

Kwa kujibu wa Mhe Balozi Dk Batilda, gari hilo kutoka Dar es Salaam kwenda Moshi, lililobeba abiria ambao idadi yao haijajulika, lilipinduka kwenye kijiji cha Chang'ombe, hivyo wakazi wake  na wale wa kijiji jirani Cha Maili Kumi, kwenda kushiriki uokozi.

Wakiwa katika kutekeleza azma hiyo, Mhe Balozi Dk Batilda anasema, ndipo roli hilo likisadikiwa kukata breki, lilipoteza mwelekeo na kwenda eneo waliokuwa wanakijiji wanaokisiwa kufikia 50 na kuwagonga baadhi yao.

Mhe Balozi Dk Batilda, amesma Serikali inachukua hatua mbalimbali kuhakikisha kasoro zilizopo kwenye barabara ya Chalinze – Segera zinarekebishwa, ili kukidhi mahitaji ya sasa yaliyo tofauti na ilivyokuwa miaka ya 1980 ilipojengwa.

Amesema,  watu waliokufa, wengi wao wakiwa ni vijana, walikuwa na nia njema ya njema na mioyo yenye huruma kuwasaidia majeruhi, lakini wakajikuta wanapoteza maisha.

Hoja hiyo inathibitishwa na majeruhi, Faraja Abdallah, mkazi wa mkazi wa Maili Kumi, aliyelazwa hospitali ya Magungu, kufuatia kujeruhiwa huku ‘akiwapoteza’ jamaa zake watano waliofariki.

Mganga wa Mfawidhi wa Hospitali ya Magunga - Korogwe, Dk Paul Patrick amethibitisha kupokea miili ya watu 11 na majeruhi 13.

Amesema hadi kufikia leo asubuhi, miili nane ilikuwa imetambuliwa wakati majeruhi saba wanapelekwa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tanga - Bombo kwa matibabu zaidi.

Mashuhuda kadhaa wameelezea namna ajali hiyo ilivyotokea na kugharimu maisha ya watu, wengi wao wakiwa ni vijana kutoka katika vijiji vya Chang’ombe na Maili Kumi.

Ester Bonifas ni mmoja wa majeruhi wa ajali ya gari aina ya Tata, anasema abiria wengi (hakutaja idadi) waliosafiri kutoka Dar es Salaam walishukia Segera, umbali wa kilomita 4.2 hadi Chang’ombe palipotokea ajali hiyo, na kuingia wengine waliokaribia kwa idadi ya walioshuka.

Naye Zaituni Njala, mkazi wa Chang’ombe amesema familia yao ilipata taarifa ya kifo cha kijana wao,  Nassib Waziri (35) waliokuwa wanamtegemea katika mahitaji yao.

‘’Tuna majonzi sana, nguvu kazi na tegemea letu ameondoka,’’ anasema kwa huzuni akiwa nje ya chumba cha maiti kwenye hospitali ya Magunga.

Mohamed Mwakigonda, mkazi wa Maili Kumi anasema, ajali nyingi zimeshuhudiwa kutokea kwenye eneo hilo, hivyo kutoa rai kwa mamlaka husika kuwekeza zaidi katika ukaguzi wa magari ikiwemo mifumo ya breki.

Kwa upande mwingine, miongoni mwa wakazi wa vijiji hivyo wamefika kwenye eneo la ajali, wakitafuta vitu wanavyovitambua kuwa vya ndugu zao waliofariki ama kujeruhiwa.

Miongoni mwao walionekana wakiokota viatu, wakidai kuwa vilivaliwa na ndugu zao wakati wakienda kwenye eneo la tukio.

Mwisho

  

Matangazo

  • MATOKEO YA MTIHANI WA KIDATO CHA NNE (CSEE)2023 January 25, 2024
  • HOTUBA YA MKUU WA MKOA WA TANGA MHE. WAZIRI WAZIRI KINDAMBA KATIKA HAFLA YA UFUNGUZI WA KONGAMANO LA UWEKEZAJI NA UZINDUZI WA MWONGOZO WA FURSA ZA UWEKEZAJI MKOA WA TANGA 16/11/2023 November 27, 2023
  • FORM ONE SELECTION 2024 December 20, 2023
  • TANGA REGION INVESTMENT GUIDE November 24, 2023
  • Angalia zote

Habari mpya

  • SAFARI YA RAIS SAMIA KWA SGR YAIBUA HISIA ZA WAKAZI WA TANGA

    May 17, 2025
  • CCM TANGA YATETA SAFARI ZA RAIS SAMIA NJE YA NCHI

    May 16, 2025
  • DC LUSHOTO ASEMA NIDHAMU, UADILIFU NI NYENZO ZA UFANISI MIRADI YA PEMBEZONI

    May 16, 2025
  • CCM: TUSIWE 'WANYAMPALA' KATIKA KUKAGUA MIRADI YA MAENDELEO

    May 16, 2025
  • Angalia zote

Video

KATIBU TAWALA MKOA WA TANGA AKIONGOZA WATUMISHI WA MKOA HUO KUFANYA MAZOEZI YA PAMOJA KATIKA UWANJA WA MKWAKWANI KUITIKIA WITO WA MHE. MAKAMU WA RAIS
Video zaidi

Viunganishi vya haraka

Tovuti zinazoendana

  • TAMISEMI
  • Kupata huduma za kiutumishi
  • Wakala ya Serikali Mtandao
  • Utumishi
  • Baraza la Mitihani Tanzania (NECTA)
  • Tovuti ya Serikali

Kifuatilia watazamaji duniani

world map hits counter

idadi ya watazamaji

free HitCounter

Ramani ya Mkoa wa Tanga

Wasiliana nasi

    Golf Area/Masiwani Road Tanga

    Anuani ya posta: P.O.Box 5095 Tanga

    Simu: 027 2642421

    Simu ya Mkononi:

    Barua pepe: ras.tanga@tamisemi.go.tz

Anuani zingine

   

    • Sera za faragha
    • Kanusho
    • Maswali na Majibu
    • Ramani ya Tovuti
    • Huduma

Haki miliki ©2017 Katibu Tawala Mkoa wa Tanga . Haki zote zimehifadhiwa.