KATIBU Tawala Mkoa wa Tanga, Pili Mnyema, amekutana na wakaguzi wa ndani na waweka hazina kutoka halmashauri 11 za mkoa huo, ili kujadili masuala ya ukusanyaji mapato na ukaguzi wenye tija zaidi.
Kikao hicho kimefanyika leo Desemba 6, 2024 kwenye ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa ambapo Mnyema, pamoja na mambo mengine, amewahimiza watumishi hao kuwajibika kwa misingi ya weledi katika majukumu yao, ili kuleta ufanisi kwenye taasisi wanapofanyia kazi.
Mnyema ametoa mfano wa uwajibikaji huo kuwa ni wakaguzi kuwa na weledi wa kuona upungufu mapema, na kutoa ushauri kwa hatua zinazohitajika ili kuboresha usimamizi wa fedha za umma.
Amesema, wakaguzi ni “jicho la taasisi” na wanatakiwa kufanya kazi kwa umakini, ili kuzuia ubadhirifu na kuhakikisha matumizi bora ya rasilimali za umma.
Aidha, amewahimiza kutekeleza wajibu wao kwa wakati, ikiwemo kujibu hoja za Mkaguzi Mkuu wa Serikali kwa haraka ili kuepuka kuchelewa kwa michakato ya fedha na masuala ya utawala.
Golf Area/Masiwani Road Tanga
Anuani ya posta: P.O.Box 5095 Tanga
Simu: 027 2642421
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ras.tanga@tamisemi.go.tz
Haki miliki ©2017 Katibu Tawala Mkoa wa Tanga . Haki zote zimehifadhiwa.