Na Mashaka Mgeta, MOROGORO
WAZIRI Mkuu Mstaafu, Mizengo Pinda, kesho atayafungua rasmi Maonesho ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi maarufu kama Nanenane ambayo kwa Kanda ya Mashariki, yanafanyika mkoani Morogoro.
Maonesho hayo ambayo kwa Kanda hiyo inayojumuisha mikoa ya Dar es Salaam, Pwani, Tanga na Morogoro, yana kauli mbiu inayosema, ‘Chagua Viongozi Bora kwa Maendeleo Endelvu ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi’.
Leo Agosti 1, 2025, Katibu Tawala Mkoa wa Tanga, Rashid Mchatta, kwa niaba ya Makatibu Tawala wa Mikoa hiyo, amekagua na kuridhishwa na utayari wa washiriki zikiwemo Halmashauri za Majiji, Manispaa, Wilaya na Miji, hivyo kuwaalika wadau wote kushiriki ipasavyo.
Mchatta amesema milango ya Viwanja vya Mwalimu Nyerere itaanza kufungulia kuanzia saa 12:30 asubuhi ambapo wananchi watatumia fursa hiyo kuzungukia mabanda, vipando na maeneo mengine yanayotoa huduma zikiwemo teknolojia zinazohusiana na sekta ya kilimo, ufugaji na uvuvi.
(Picha na Emma Kigombe, MOROGORO)
Golf Area/Masiwani Road Tanga
Anuani ya posta: P.O.Box 5095 Tanga
Simu: 027 2642421
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ras.tanga@tamisemi.go.tz
Haki miliki ©2017 Katibu Tawala Mkoa wa Tanga . Haki zote zimehifadhiwa.