Na Mashaka Mgeta, OMM TANGA
MATUNDA ya kazi ya miaka mitano ya Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Mhe Rais Dkt Samia Suluhu Hassan, yanaonekana, wakati Taifa likielekea kwenye Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2025.
Kwenye Uchaguzi huo wa saba tangu kuanza upya kwa mfumo wa vyama vingi vya siasa nchini mwaka 1992 na Uchaguzi Mkuu wa kwanza kwa mfumo huo kufanyika 1995, Mhe Rais Dkt Samia anagombea kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Mhe Balozi Dkt Batilda Burian (katikati waliokaa kwenye picha) anasema punde kampeni za Uchaguzi Mkuu zitakapoanza, viongozi wa Serikali watatimiza wajibu wao, kwa mujibu wa Sheria, Kanuni na Taratibu za uchaguzi huo.
Akizungumza kwenye Kongamano la Wafanyabiashara Ndogondogo wa mkoani jana Agosti 22, 2025, Mhe Balozi Dkt Batilda, akasema Watanzania wameshuhudia kwa maelezo na vitendo, namna Mhe Rais Dkt Samia alivyotekeleza ahadi zilizotolewa 2020, na alipoingia madarakani Machi 2021 baada ya kifo cha mtangulizi wake, hayati John Pombe Magufuli.
Amesema hatua ya Serikali kutekeleza miradi ya maendeleo na ustawi wa watu katika ngazi tofauti imefanyika kwa weledi, ikiwa ni mfano wa ’somo zuri kwa wananchi’, hivyo wajibu wao ni kumtendea haki Mhe Rais Dkt Samia Suluhu Hassan katika Uchaguzi Mkuu huo.
Afisa Maendeleo ya Jamii wa Mkoa wa Tanga, Gloria Maleo, akasema miongoni mwa hatua muhimu wa kuwatambua wafanyabiashara hao iliyofikiwa na Serikali ya Mhe Rais Dkt Samia ni utambuzi unaofanyika kwa mifumo ya kielektroniki.
Hata hivyo, amesema zipo changamoto kadhaa zikiwemo uelewa duni kuhusu mifumo hiyo, kutopokea mabadiliko kwa haraka, kiwango kidogo cha ubunifu kinachopunguza uzalishaji na masoko.
Changamoto hizo zinazotolewa pia kupitia risala ya Wafanyabiashara Ndogondogo zinachukuliwa na Mhe Balozi Dkt Batilda kwa uzito na kuzifanyia kazi.
Kwenye kongamano hilo, mabenki na taasisi mbalimbali za fedha ziliwasilisha fursa za mikopo inayotolewa kwa ajili ya wafanyabiashara hao.
Golf Area/Masiwani Road Tanga
Anuani ya posta: P.O.Box 5095 Tanga
Simu: 027 2642421
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ras.tanga@tamisemi.go.tz
Haki miliki ©2017 Katibu Tawala Mkoa wa Tanga . Haki zote zimehifadhiwa.