• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali na Majibu |
    • Barua pepe |
Tanga Region
Tanga Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Tanga

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Dira na Dhima
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za maji
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
    • Idara
      • Utawala na Utumishi
      • Mipango na Uratibu
      • Miundombinu
      • Elimu
      • Afya
      • Maji
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Usimamizi wa Serikali za Mitaa
    • Vitengo
      • TEHAMA
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa ndani
      • Manunuzi
      • Sheria
  • Machapisho
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu za Maombi
    • Hotuba
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Sehemu ya picha
    • Habari
    • Matukio
  • Miradi
    • Miradi iliyokamilika
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya Pangani
    • Halmashauri ya Wilaya Mkinga
    • Halmashauri ya Wilaya Muheza
    • Halmashauri ya Jiji Tanga
    • Halmashauri ya Wilaya Korogwe
    • Halmashauri ya Mji Korogwe
    • Halmashauri ya Wilaya Handeni
    • Halmashauri ya Mji Handeni
    • Halmashauri ya Wilaya Kilindi
    • Halmashauri ya Wilaya Lushoto

RC BATILDA AINGIA TANGA…ATAJA VIPAUMBELE 14

Imewekwa tarehe: March 13th, 2024

RC BATILDA AINGIA TANGA…ATAJA VIPAUMBELE 14 

Na Mashaka Mgeta, TANGA

MKUU wa Mkoa wa Tanga, Balozi Dk Batilda Burian, ametaja vipaumbele 14 vitakavyomuongoza katika utumishi wake mkoani humo.

Mhe Dk Batilda amehamishiwa Tanga akitokea Tabora alipokuwa katika wadhifa huo, baada ya Mheshimiwa Rais Dk Samia Suluhu Hassan kufanya uteuzi na kuwabadilishia vituo vya kazi baadhi ya viongozi wa kuteuliwa Machi 9, 2024.

Mhe Dk Batilda amechukua nafasi hiyo kutoka kwa mtangulizi wake, Waziri Kindamba, aliyeteuliwa kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Mabasi Yaendayo Haraka (UDART).

Akizungumza katika hafla ya kumuapisha Mkuu wa Wilaya ya Mkinga, Mhe Evans Mtambi, Mhe Dk Batilda amevitaja vipaumbele hivyo kuwa ni kukuza kiwango cha elimu hasa katika ufaulu, uboreshaji wa huduma za afya na sekta ya kilimo na uvuvi.

Pia Mhe Dk Batilda amevitaja vipaumbele vingine ni miradi ya kimkakati na ubunifu wa fursa zinazotokana na miradi hiyo, ulinzi na usalama wa watu na mali zao, udhibiti wa mfumko wa bei hasa kipindi hiki cha mfungo wa Kwaresma na Ramadhani.

Mhe Dk Batilda amevitaja vipaumbele vingine kuwa ni kusikiliza na kutatua kero za wananchi, uimarishaji wa majukwaa ya uwezeshaji, utatuzi wa migogoro ya ardhi, usafi na hifadhi ya mazingira.

Vipaumbele vingine ni usimamizi wa maadili mema kwa jamii, lishe hasa kwa watoto wa chini ya miaka mitano na wanafunzi mashuleni, Mwenge wa Uhuru 2024 na uchaguzi wa serikali za mitaa, vijiji na vitongoji.

Amesema mafanikio katika kuleta ufanisi kwenye vipaumbele hivyo yanategemea zaidi ushirikiano na kutimiza wajibu kwa kila mtumishi wa umma mkoani humo.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Muheza, Mhe Zainab Abdallah amesema, uzoefu wa kitaaluma na kazi alizozifanya Mhe Dk Batilda vinatarajiwa kuwa nyenzo za kuchagiza kasi ya maendeleo na ustawi wa wananchi wa Tanga.

Mhe Zainab amesema wakuu wa wilaya, wakurugenzi watendaji wa halmashauri na watumishi wote wa umma kwenye wilaya nane za mkoani humo, wapo tayari kutoa ushirikiano, kupokea na kutekeleza maelekezo ya Mhe Dk Batilda, ili kufikia malengo ya utekelezaji wa Ilani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Mwenyekiti wa Mkoa wa CCM, Ustaadhi Rajab Abdulrahaman amesema mabadiliko yanayofanywa na Mhe Dk Samia yamezidi kuineemesha Tanga kwa kuwa na viongozi wenye kutekeleza maono yake (Mhe Rais Dk Samia) katika kuwatumikia wananchi.

Ustaadhi Rajab amesema miongoni mwa maeneo ambayo CCM inatarajia kuona yakifanyiwa kazi kwa nguvu zaidi ni usafi na uhifadhi wa mazingira, hasa kwenye masoko ambapo hali ilibainika kuwa si ya kuridhisha.

Matangazo

  • MATOKEO YA MTIHANI WA KIDATO CHA NNE (CSEE)2023 January 25, 2024
  • HOTUBA YA MKUU WA MKOA WA TANGA MHE. WAZIRI WAZIRI KINDAMBA KATIKA HAFLA YA UFUNGUZI WA KONGAMANO LA UWEKEZAJI NA UZINDUZI WA MWONGOZO WA FURSA ZA UWEKEZAJI MKOA WA TANGA 16/11/2023 November 27, 2023
  • FORM ONE SELECTION 2024 December 20, 2023
  • TANGA REGION INVESTMENT GUIDE November 24, 2023
  • Angalia zote

Habari mpya

  • HISTORIA YAANDIKWA, HANDENI YAPATA CHUO CHA UUGUZI NA UKUNGA

    May 04, 2025
  • SPIKA BWZ AGAWA MITUNGI YA GESI 61 KUADHIMISHA MIAKA 61 YA MUUNGANO

    April 27, 2025
  • SPIKA BWZ ATEMBELEA MIRADI YA BILIONI 8 TANGA

    April 26, 2025
  • MILIONI 100 ZATOLEWA KUBORESHA SOKO LA NGAMIANI TANGA

    April 26, 2025
  • Angalia zote

Video

KATIBU TAWALA MKOA WA TANGA AKIONGOZA WATUMISHI WA MKOA HUO KUFANYA MAZOEZI YA PAMOJA KATIKA UWANJA WA MKWAKWANI KUITIKIA WITO WA MHE. MAKAMU WA RAIS
Video zaidi

Viunganishi vya haraka

Tovuti zinazoendana

  • TAMISEMI
  • Kupata huduma za kiutumishi
  • Wakala ya Serikali Mtandao
  • Utumishi
  • Baraza la Mitihani Tanzania (NECTA)
  • Tovuti ya Serikali

Kifuatilia watazamaji duniani

world map hits counter

idadi ya watazamaji

free HitCounter

Ramani ya Mkoa wa Tanga

Wasiliana nasi

    Golf Area/Masiwani Road Tanga

    Anuani ya posta: P.O.Box 5095 Tanga

    Simu: 027 2642421

    Simu ya Mkononi:

    Barua pepe: ras.tanga@tamisemi.go.tz

Anuani zingine

   

    • Sera za faragha
    • Kanusho
    • Maswali na Majibu
    • Ramani ya Tovuti
    • Huduma

Haki miliki ©2017 Katibu Tawala Mkoa wa Tanga . Haki zote zimehifadhiwa.