Na Emma Kigombe, OMM TANGA
MKUU wa Mkoa wa Tanga, Mhe. Dkt. Batilda Burian, amezindua Kampeni ya Kitaifa ya Chanjo ya Mifugo katika viwanja vya Chuo cha Mafunzo ya Mifugo (LITA – Buhuri) jana Agosti 20, 2025.
Mhe Balozi Dkt Batilda amesema Tanga imejipanga kuchanja zaidi ya mifugo milioni mbili ili kudhibiti magonjwa na kuongeza tija katika sekta hiyo muhimu kwa maendeleo ya wananchi na uchumi wa taifa.
Amesema, kampeni hiyo ni sehemu ya utekelezaji wa mkakati wa kitaifa wa kulinda na kuendeleza rasilimali za mifugo, uliozinduliwa na Mhe Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, Juni 16, 2025 mkoani Simiyu.
Alisisitiza kuwa chanjo ya mifugo ni nyenzo muhimu katika usalama wa chakula, ustawi wa jamii, afya ya binadamu na utunzaji wa mazingira.Mhe Balozi Dkt. Batilda amesema kuwa kwa Mkoa wa Tanga pekee, kampeni hiyo inalenga kuchanja ng’ombe 668,000 , mbuzi na kondoo 1,055,700 na kuku 1,162,200 hatua ambayo inalenga kuimarisha afya ya mifugo, na kuzuia milipuko ya magonjwa ambayo huathiri uzalishaji na maisha ya wananchi wengi wanaotegemea sekta hiyo kwa kipato.
Aidha, alieleza kuwa mkoa huo umepokea vifaa muhimu vya kutekeleza kampeni hiyo, ikiwa ni pamoja na dozi za chanjo, vishikwambi, barafu za kuhifadhia chanjo, sindano, hereni za mifugo na mavazi ya kujikinga kwa wataalamu wa afya ya mifugo.Katika hatua nyingine, Mge Balozi Dkt. Batilda ametoa wito kwa wafugaji kuhakikisha mifugo yao inafikishwa katika vituo vya chanjo, vilivyopangwa katika maeneo yao ili kuhakikisha kampeni hiyo inafanikiwa kwa asilimia 100.
Golf Area/Masiwani Road Tanga
Anuani ya posta: P.O.Box 5095 Tanga
Simu: 027 2642421
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ras.tanga@tamisemi.go.tz
Haki miliki ©2017 Katibu Tawala Mkoa wa Tanga . Haki zote zimehifadhiwa.