Na Mashaka Mgeta, OMM TANGA
MKUU wa Mkoa wa Tanga, Mhe Balozi Dkt Batilda Burian, amesema uongozi mkoani Tanga unatekeleza maelekezo ya Mhe Rais Dkt Samia Suluhu Hassan, ili kufikia lengo la kuwafanya wakazi wake kuwa na maisha bora zaidi.
Mhe Balozi Dkt Batilda, akifuatana na Katibu Tawala Mkoa, Pili Mnyema na wajumbe Kamati ya Usalama (KU) ya mkoa huo, wameshiriki kilele cha mbio za Mwenge wa Uhuru 2025 mkoani humo, ambao usiku huu unakesha kwenye eneo la Kisosora.
Mhe Balozi Dkt Batilda amesema Mhe Rais Dkt Samia ametimiza ahadi zake nyingi katika kuwahudumia Watanzania wakiwemo wakazi wa Tanga wanaonufaika na ahadi ya kuirejesha Tanga ya viwanda.Amesema, matunda ya ahadi za Mhe Rais Dkt Samia zinaonekana, akitoa mfano wa kasi ya kujengwa ama kufufuka kwa viwanda vilivyotoweka.
Mhe Balozi Dkt Batilda amesema pia kuwa, uwekezaji unaokolezwa na ujenzi wa miundombinu kama bandari ya Tanga na huduma za kijamii zikiwemo afya, elimu, nishati nakadhalika ni miongoni mwa viashiria vya utekelezaji wa ahadi za Mhe Rais Dkt Samia.Kesho Juni 17, 2025,
Mwenge wa Uhuru wenye ujumbe unaosema, JITOKEZE KUSHIRIKI UCHAGUZI MKUU WA 2025 KWA AMANI NA UTULIVU, utapelekwa Zanzibar.
Golf Area/Masiwani Road Tanga
Anuani ya posta: P.O.Box 5095 Tanga
Simu: 027 2642421
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ras.tanga@tamisemi.go.tz
Haki miliki ©2017 Katibu Tawala Mkoa wa Tanga . Haki zote zimehifadhiwa.