WAKALA wa Misitu Tanzania (TFS) imetoa mizinga 100 kwa wakazi wa kijiji cha Msomera wilayani Handeni, ikiwa ni kuunga mkono jitihada zao kukuza shughuli za kiuchumi, kuhifadhi na kulinda misitu.
Mizinga hiyo yenye thamani ya Shilingi milioni 10 ni sehemu ya mizinga 200 iliyoahidiwa na Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Mhe Waziri Kindamba katika ziara yake ya kikazi hivi karibuni wilayani Handeni.
Taarifa iliyotolewa na Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Uhifadhi wa TFS Kanda ya Kaskazini, James Nshare, imeeleza kuwa mizinga hiyo inaelekezwa kwenye vikundi vitatu vya awali vya Ewechena, Naiboshu na Datoga.
Ameitaja misitu itakayotumika kwa vikundi hivyo kufugia nyuki ni Osojo (hekta 9.4), Msomera (hekta 12.9) na Anatwangaina (hekta 32).
Naye Mhe Kindamba amewahimiza wakazi wa Msomera kutumia mizinga hiyo kama nyenzo muhimu katika uhifadhi wa misitu.
Habari hii imeandikwa na Mashaka Mgeta wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Tanga
Golf Area/Masiwani Road Tanga
Anuani ya posta: P.O.Box 5095 Tanga
Simu: 027 2642421
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ras.tanga@tamisemi.go.tz
Haki miliki ©2017 Katibu Tawala Mkoa wa Tanga . Haki zote zimehifadhiwa.