Na Mashaka Mgeta, SAADANI
MKUU wa Mkoa wa Tanga, Mhe Balozi Dkt. Batilda Burian, amewataka watumishi wa umma mkoani humo, kujiepusha na vitendo vinavyoashiria ama kusababisha kadhia kwa wananchi wanaofika kupata huduma kwenye maeneo yao.
Mhe Balozi Dkt Batilda, ameyasema hayo wakati akifunga kikao cha Baraza la Wafanyakazi mkoani Tanga, kilichofanyika jana Januari 27, 2026 kwenye Hifadhi ya Taifa ya Saadani.
Amesema, pamoja na mwenendo mzuri wa kujivunia kwa utumishi wa umma kwa utoaji huduma wenye kuridhisha mkoani humo, ipo haja ya kuendeleza utendaji kazi unaojali utu, weledi na maadili katika hatua zote zinazohusiana na utendaji kazi wao.
“Tuyatekeleze haya mahali popote tunapotoa huduma, kama ni ofisini basi iwe tangu mwananchi anapoingia getini, anavyopokewa, lugha na matendo yetu visiwe vyenye kusababisha kadhia kwao,” amesema.
Pia, Mhe Balozi Dkt. Batilda amewahimiza watumishi katika Sekretarieti ya Mkoa (RS) kuimarisha zaidi mifumo na ufuatiliaji wa miradi na huduma zinazotolewa na Serikali, ili kukidhi thamani ya fedha zinazotolewa.
Naye Katibu Tawala Mkoa wa Tanga, Rashid Mchatta, alisem a wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi, walijadili kwa kina, uhuru na uwazi masuala yanayowahusu katika kufikia malengo ya Serikali kuwatumikia wananchi.
Alisema, watumishi wa umma kutoka idara na vitengo vyote wamethibitisha kutambua na nafasi na umuhimu wa majukumu yao, hivyo kuahidi kuendelea kuwajibika kadri ya maadili ya utumishi wa umma.
Golf Area/Masiwani Road Tanga
Anuani ya posta: P.O.Box 5095 Tanga
Simu: 027 2642421
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ras.tanga@tamisemi.go.tz
Haki miliki ©2017 Katibu Tawala Mkoa wa Tanga . Haki zote zimehifadhiwa.