Serikali Wilayani Korogwe Mkoani Tanga imempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuona umuhimu wa kuendeleza zaidi sekta ya elimu na kuboresha miundombinu yake ili kuwawekea mazingira rafiki wanafunzi kuweza kujifunza.
Pongezi hizo zimetolewa na Katibu Tawala wa Wilaya ya Korogwe Rahel Mhando ambae alimwakilisha Mkuu wa wilaya hiyo katika ufunguzi wa mafunzo ya Mradi wa Shule Bora kwa waandishi wa habari wa Mkoa wa Tanga uliofanyika wilayani humo.
“Ari kubwa ya Mhe. Rais ni kuhakikisha kuwa na miundombinu ya uhakika kuwatosheleza wanafunzi kuweza kusoma katika mazingira mazuri alisema Mhando.
Aidha Mhando alimpongeza Rais Dkt Samia kwa kuahirisha sherehe za Maadhimisho ya Uhuru na kuzipeleka fedha hizo kwenye ujenzi wa mabweni katika shule mbalimbali nchini.
Naye Afisa Elimu wa mkoa wa Tanga Niwaho Mkisi amewataka waandishi wa habari waliopata mafunzo kuhakikisha kwa pamoja wanautangaza mradi wa shule bora kwa kuleta manufaa na mageuzi makubwa katika sekta ya elimu nchini.
Mradi wa Shule Bora umelenga kuinua kiwango cha elimu jumuishi pamoja na kuweka mazingira salama na rafiki katika shule za serikali za awali na msingi nchini, ambapo kiasi cha shilingi Bilioni 271 zitatumika katika utekelezaji wa mradi mpaka ifikapo 2027.
Mwisho
Golf Area/Masiwani Road Tanga
Anuani ya posta: P.O.Box 5095 Tanga
Simu: 027 2642421
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ras.tanga@tamisemi.go.tz
Haki miliki ©2017 Katibu Tawala Mkoa wa Tanga . Haki zote zimehifadhiwa.