WIZARA ya Afya kwa kushirikiana na Ofisi ya Rais (TAMISEMI) inatekeleza mpango wa matibabu ya awali kwa wahudumu wa afya ngazi ya jamii 440, kupitia taasisi ya Benjamin Mkapa.
Kupitia mpango huo, wahudumu hao wamepewa vifaa tiba vitakavyosaidia kuboresha huduma kwa wakazi wa halmashauri za jiji la Tanga na Handeni Mji, hivyo kubaini na kupunguza changamoto zinazohusiana na masuala ya afya.
Kwa mkoa wa Tanga, mpango huu unaofadhiliwa na Ireland, unagharimu zaidi ya Shilingi milioni 122 na tayari umeshatekelezwa katika mikoa 12 na halmashauri 21 nchini.
Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Mhe Balozi Dk Batilda Burian, amesema mpango huo utaboresha afua za lishe na afya kwa jamii.
Aidha, amewaagiza wahudumu hao kutekeleza majukumu yao kwa weledi, ili kufanikisha lengo la Serikali la kuboresha afya kwa wote.
Baadhi ya huduma zitakazotolewa kupitia mpango huu ni pamoja na elimu ya afya kwa jamii, huduma za kinga, afya ya mama, mtoto na vijana, huduma tembezi ya mkoba, pamoja na matibabu ya magonjwa ya kuambukiza.
Kupitia mpango huo, wananchi wanatarajiwa kupata huduma bora zaidi za afya moja kwa moja katika jamii zao, hivyo kuimarisha ustawi wa afya nchini.
Golf Area/Masiwani Road Tanga
Anuani ya posta: P.O.Box 5095 Tanga
Simu: 027 2642421
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ras.tanga@tamisemi.go.tz
Haki miliki ©2017 Katibu Tawala Mkoa wa Tanga . Haki zote zimehifadhiwa.