Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la ndege nchini Ladislaus Matindi amesema hayo mara baada ya ziara yake ya aiku moja kukagua Uwanja wa Ndege huo kwaajili ya kupokea ndege kubwa.
Naye Mkuu wa Mkoa wa Tanga Adam Malima alisema kuwa kuboreshwa kwa uwanja wa Tanga kutawezesha Mkoa wa Tanga kuwa kiunganishi wa safari za ndege kutoka mikoa mingine jambo ambalo pia itafungua uchumi wa kiutali kwa kaisi kubwa zaidi.
"Ujenzi wa miradi ya kimkakati Mkoani Tanga ikiwemo upanuzi wa Bandari pamoja na Bomba la Mafuta utaongeza fursa za wawekezaji ambao watatumia safari za anga mara kwa mara" amefafanua zaidi.
Picha: Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Ndege Tanzania (ATCL) Mhandisi Ladislaus Matindi, akimwonyesha Mkuu wa Mkoa wa Tanga Adam Malima ( kulia ) ukubwa wa eneo la Uwanja wa Ndege wa Tanga linalotakiwa katika upanuzi wa kiwanja hicho ili ndege kubwa ziweze kutua
Golf Area/Masiwani Road Tanga
Anuani ya posta: P.O.Box 5095 Tanga
Simu: 027 2642421
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ras.tanga@tamisemi.go.tz
Haki miliki ©2017 Katibu Tawala Mkoa wa Tanga . Haki zote zimehifadhiwa.