• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali na Majibu |
    • Barua pepe |
Tanga Region
Tanga Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Tanga

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Dira na Dhima
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za maji
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
    • Idara
      • Utawala na Utumishi
      • Mipango na Uratibu
      • Miundombinu
      • Elimu
      • Afya
      • Maji
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Usimamizi wa Serikali za Mitaa
    • Vitengo
      • TEHAMA
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa ndani
      • Manunuzi
      • Sheria
  • Machapisho
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu za Maombi
    • Hotuba
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Sehemu ya picha
    • Habari
    • Matukio
  • Miradi
    • Miradi iliyokamilika
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya Pangani
    • Halmashauri ya Wilaya Mkinga
    • Halmashauri ya Wilaya Muheza
    • Halmashauri ya Jiji Tanga
    • Halmashauri ya Wilaya Korogwe
    • Halmashauri ya Mji Korogwe
    • Halmashauri ya Wilaya Handeni
    • Halmashauri ya Mji Handeni
    • Halmashauri ya Wilaya Kilindi
    • Halmashauri ya Wilaya Lushoto

SHULE YA SEKONDARI YA MKOA WA TANGA KUANZA KUPOKEA WANAFUNZI WA KIDATO CHA TANO MWEZI JULAI

Imewekwa tarehe: June 10th, 2024

Katibu Tawala Mkoa wa Tanga Pili Mnyema tarehe 3 Juni, 2024 amefanya ziara ya kutembelea na kukagua hatua ya mradi wa ujenzi wa Shule ya Sekondari ya wasichana ya Mkoa wa Tanga (Tanga girls) inayojengwa katika eneo la Mabalanga wilayani Kilindi.

Akizungumza mara baada ya kukagua ujenzi wa Shule hiyo Katibu Tawala amesema Serikali imetoa fedha kiasi cha shilingi Bilioni Tatu  kwa ajili ya ujenzi wa Shule  ya Mkoa  ya wasichana lengo likiwa kuweka mazingira rafiki kwa watoto wa kike kupata Elimu bora na kuhamasisha  kusoma masomo ya sayansi.

Mnyema amewataka viongozi wa Halmashauri ya wilaya ya Kilindi  na mwananchi wa mabalanga kusimamia mradi huo kwa ushirikiano mkubwa ili kuhakikisha unakamilika kwa wakati  na  kufanya kazi iliyokusudiwa na Mhe Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ya kumpatia Elimu bora mtoto wa kike.

Mradi wa ujenzi wa Shule ya wasichana ya mkoa wa Tanga una jumla ya madarasa 12, mabweni nane, jengo la utawala, maabara tatu, nyumba za walimu , chumba cha wagonjwa, matundu ya vyoo ambapo vipo katika hatua ya umaliziaji pamoja na bwalo la chakula liliofikia asilimia 70.

Shule ya Sekondari ya wasichana ya Mkoa wa Tanga inatarajia kupokea kwa mara ya kwanza wanafunzi wa kidato cha Tano 122 kwa michepuo ya sayansi mapema mwezi Julai mwaka huu.

Matangazo

  • TANGA REGION INVESTMENT GUIDE November 24, 2023
  • SENSA YA WATU NA MAKAZI MWAKA 2022 MKOA WA TANGA June 13, 2023
  • Angalia zote

Habari mpya

  • SARUJI TANGA YAKABIDHI BAJAJI ZA UMEME 10 KWA BALOZI BATILDA

    July 03, 2025
  • RC TANGA ASULUHISHA MGOGORO WA ARDHI TAFSIRI HASI YA RAMANI IKITAJWA CHANZO

    July 03, 2025
  • RAS MCHATTA: SINA MANENO MENGI, NIPIMENI KWA KAZI, UWAJIBIKAJI

    June 30, 2025
  • BALOZI BATILDA AAGIZA WAKUU WA WILAYA KUSIKILIZA KERO, AWAAPISHI WAWILI TANGA

    June 30, 2025
  • Angalia zote

Video

KATIBU TAWALA MKOA WA TANGA AKIONGOZA WATUMISHI WA MKOA HUO KUFANYA MAZOEZI YA PAMOJA KATIKA UWANJA WA MKWAKWANI KUITIKIA WITO WA MHE. MAKAMU WA RAIS
Video zaidi

Viunganishi vya haraka

Tovuti zinazoendana

  • TAMISEMI
  • Kupata huduma za kiutumishi
  • Wakala ya Serikali Mtandao
  • Utumishi
  • Baraza la Mitihani Tanzania (NECTA)
  • Tovuti ya Serikali

Kifuatilia watazamaji duniani

world map hits counter

idadi ya watazamaji

free HitCounter

Ramani ya Mkoa wa Tanga

Wasiliana nasi

    Golf Area/Masiwani Road Tanga

    Anuani ya posta: P.O.Box 5095 Tanga

    Simu: 027 2642421

    Simu ya Mkononi:

    Barua pepe: ras.tanga@tamisemi.go.tz

Anuani zingine

   

    • Sera za faragha
    • Kanusho
    • Maswali na Majibu
    • Ramani ya Tovuti
    • Huduma

Haki miliki ©2017 Katibu Tawala Mkoa wa Tanga . Haki zote zimehifadhiwa.