Na Mashaka Mgeta, OMM TANGA
SPIKA wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar, Mhe Zubeir Ali Maulid, leo Aprili 24, 2025, amewasili mkoani Tanga kwa ziara ya siku nne.
Katika ziara hiyo iliyo sehemu ya matendo ya kuadhimisha miaka 61 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar, Mhe Maulid, amepokewa na Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Mhe Balozi Dkt Batilda Burian.
Pia walikuwepo Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wa Mkoa wa Tanga, Rajabu Abdulrahman Abdallah na Mbunge wa Mkinga ambaye pia ni Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe Dustan Kitandula. Mhe Maulid ameelezea matumaini ya ziara yake hiyo ya kwanza ya kikazi, kuwa yenye tija.
Naye Mhe Balozi Dkt Batilda Burian amesema, miongoni mwa kazi atakazozifanya Mhe Maulid ni ukakuguzi, kuweka jiwe la msingi, kufungua miradi ya maendeleo na kuwahutubia wakazi wa maeneo atakayoyatembelea.
Mhe Balozi Dkt Batilda amesema, Tanga imepokea zaidi ya Shilingi trilioni 3.1 zilizotolewa na Mhe Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa ajili miradi ya maendeleo na ustawi wa watu.
Golf Area/Masiwani Road Tanga
Anuani ya posta: P.O.Box 5095 Tanga
Simu: 027 2642421
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ras.tanga@tamisemi.go.tz
Haki miliki ©2017 Katibu Tawala Mkoa wa Tanga . Haki zote zimehifadhiwa.