Na Mashaka Mgeta, OMM TANGA
MAELFU ya wakazi wa mkoani Tanga, leo Desemba 31, 2025, wameingia siku ya nne ya Tamasha la Urithi Tanga kwa kumuombea dua Mhe Rais Dk Samia Suluhu Hassan; na Tanzania kwa ujumla.
Viongozi 20 wa madhehebu na taasisi za dini mbalimbali, wamewaongoza wakazi hao waliokutana kwenye viwanja vya ‘Urithi Wetu’, wakiwa na Mkuu wa Mkoa, Mhe Balozi Dk Batilda Burian na Katibu Tawala Mkoa, Pili Mnyema.
Viongozi hao na taasisi husika kwenye mabano ni Shehe wa Mkoa, Juma Luwuchu (Mwenyekiti wa Kamati ya Amani Mkoa), Mchungaji Samwel William (Nayothi Assemblies of God), Mchungaji Leonard Haule (Bethania Christian Church), Wachungaji Anton Mwaisaka na Lucas Stephen (PAG), Shehe Omar Sinde ( Fadhila Njombe Mpirani), Mchungaji Elizabeth Bayo (Bethan – Donge), Mchungaji Daniel Msumary (Katibu wa Kamati ya Amani Mkoa) na Mtumishi Richard Meda (Kanisa la Jesami),
Wengine ni Shehe Juma Bakari (Katibu wa Baraza la Mashehe Mkoa), Shehe Ayoub Yusuph (Mwenyekiti wa Halmashauri ya BAKWATA Mkoa), Shehe Alhaj Bawazir (Mwenyekiti wa Wazee Tanga), Shehe Mohamed Dhikri (Katibu TAMTA), Shehe Musa Kunema (Mwenyekiti Shamsi Maarifa), Shehe Baamini (Mkuu wa Madrasa Irishadi), uongozi wa Zahra Madrasa na Shehe Musa Faki (Naibu Jahamia Islamia) na Wachungaji Gabriel Christopher, Andrew Mndeme na Henry Mnango (Sabato),
Shehe Luwuchu amesema umuhimu wa dua kwa Mhe Rais Dk Samia, unatokana na ukubwa na uzito wa kazi na majukumu aliyonayo katika kuwaongoza raia wanaokadirwa kuwa zaidi ya milioni 60.
‘’Zipo familia zenye watoto wachache kama watatu hivi, lakini inakuwa nguvu kwa wazazi kumudu kuziongoza, sasa inakuwaje kwa Mh Rais anayewaongoza Watanzania zaidi ya milioni 60….tunapaswa kumuombea na kuiombea nchi yetu,’’ amesema.
Shehe Luwuchu amesema, uhakika wa taifa kuwa na utulivu endelevu utapatikana ikiwa wazazi na walezi watawekeza katika kuwalea na kuwaelekeza watoto katika misingi ya amani ya kudumu.
Golf Area/Masiwani Road Tanga
Anuani ya posta: P.O.Box 5095 Tanga
Simu: 027 2642421
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ras.tanga@tamisemi.go.tz
Haki miliki ©2017 Katibu Tawala Mkoa wa Tanga . Haki zote zimehifadhiwa.