Na Mashaka Mgeta, OMM-TANGA
ELIMU ni miongoni mwa sekta zilizoboreka mkoani Tanga katika kipindi cha miaka mitatu ya uongozi wa Mhe Rais Dk Samia Suluhu Hassan.
Ndani ya kipindi hicho, mkoa wa Tanga umepokea Shilingi 121,015,652,154 kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu na fedha za elimu bila malipo.
Taarifa iliyotolewa na Idara ya Mipango ya Sekretarieti ya Mkoa (RS) inaeleza kuwa kupitia fedha hizo, Tanga imeongeza shule za msingi kutoka 1,054 hadi shule 1,083 wakati madarasa yameongezeka kutoka 7,048 kufikia 7,432.
Pia, taarifa hiyo inaonyesha kuwa hadi kufikia Disemba 2023, kumekuwa na ongezeko la uandikishaji darasa la awali 5,164, yaani kutoka wanafunzi 58,098 hadi 63,262 na darasa la kwanza 4,180 ikiwa ni kutoka wanafunzi 72,254 hadi 76,434.
Katika elimu ya sekondari, fedha hizo zimefanikisha ongezeko la kutoka shule kutoka 287 hadi 301 na madarasa 2,702 hadi 3629.
Kwa mchanganuo wake, taarifa inaonyesha kuwa Shilingi 21,079,114,646 zilitolewa kwa ujenzi wa madarasa 1,026 ya shule za msingi; ongezeko la madarasa 550 ikilinganishwa na 476 yaliyokuwepo awali.
Kwa upande wa sekondari,Tanga imepokea Shilingi 25,672,990,090 kwa ujenzi wa madarasa 1,225, ikiwa ni ongezeko la madarasa 927 ikilinganishwa na 298 yaliyokuwepo awali.
Fedha zilizotolewa zimetumika pia kwa ujenzi wa nyumba za walimu 40 wa shule za msingi ni Shilingi 1,850,000,000, ikiwa ni ongezeko la nyumba 25 kutoka 15 za awali.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo, Shilingi 2,177,367,943 zimetumika kujenga nyumba za walimu 41 wa sekondari, ikiwa ni ongezeko la nyumba 13 ikilinganishwa na nyumba 28 zilizojengwa katika uongozi wa awamu ya tano.
Katika mchanganuo huo, Shilingi 320,000,000 ziliwezesha ujenzi wa mabweni matano ya shule za msingi wakati Shilingi 8,757,500,000 zilitengwa kwa ujenzi wa mabweni 81 katika shule za sekondari, ikiwa ni ongezeko la mabweni 33 dhidi ya 48 ya awali. Uwepo wa shule pia unahusisha afya za wanafunzi na walimu na ndio maana katika kipindi hicho, Tanga imepokea Shilingi 5,098,118,618.14 za ujenzi wa matundu ya vyoo 3,501 katika shule za sekondari na msingi, ikiwa ni ongezeko la matundu 2,212 dhidi ya 1,289 yaliyokuwepo.
Fedha zilizotolewa mkoani Tanga katika sekta ya elimu, zilihusisha ujenzi wa maabara 157 za sekondari, uliogharimu Shilingi 5,879,526,947.27, ikiwa ni ongezeko la maabara 117 kutoka 40 zilizokuwepo awali.
Pia, Shilingi 1,130,000,000 zilizowezesha ujenzi wa mabwalo 10 katika shule za sekondari ikiwa ni ongezeko la mabwalo matatu kutoka saba yaliyokuwepo.
Taarifa hiyo inaeleza zaidi kuwa, katika kipindi cha miaka mitatu, Mhe Rais Dk Samia ametoa jumla ya Shilingi 6,580,000,000 za ujenzi wa sekondari kupitia mradi wa kuboresha elimu ya sekondari (SEQUIP) ambapo shule 14 zilinufaika kwa kutengewa Shilingi 470,000,000 kila moja.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo, matumizi mengine ya fedha za elimu mkoani Tanga ni kutengwa Shilingi 260,000,000 kwa ajili ya upanuzi wa kidato cha tano na sita katika Shule ya Sekondari ya Wasichana Korogwe.
Awamu nyingine ya fedha nyingine za SEQUIP zilitolewa Shilingi 12,089,360,336, ambapo Shilingi 1,078,000,000 kwa ajili ya ujenzi wa nyumba za watumishi (2 in 1). Kila shule kati ya 11 za kwanza ilipata Shilingi 98,000,000.
Shule nyingine 12 zilipatapa jumla ya Shilingi7, 011,360,00 kwa kila shule kugharimu Shilingi 584,280,028. Pia, Shilingi Bilioni 3 zilitolewa kwa ujenzi wa shule mpya ya wasichana ya Mkoa, inayojengwa katika wilaya ya Kilindi. Ujenzi wa shule hizi uko katika hatua mbalimbali za ujenzi.
Upanuzi wa Shule za Kidato cha Tano na SitaKiasi cha Shilingi 4,515,300,000 kiliotolewa kujenga miundombinu ya shule 10 za kidato cha tano na sita. Shule hizo ni Kisaza, Mafisa, Mkindi, Magoma, Mnyuzi, Magamba, Ubiri, Muheza, Mwera na Galanos.
Aidha, jumla ya madarasa 66 yamejengwa, mabweni 20 na matundu ya vyoo 131. Ujenzi uko katika hatua mbalimbali. Kutokana na ujenzi huo changamoto ya mabweni kwa wanafunzi imepungua.
Elimu Bila MalipoKwa kipindi cha miaka mitatu ya Mhe Rais Dk Samia madarakani, Tanga imepokea Shilingi 16,099,492,191.48 kugharamia mpango wa elimu bila malipo.
Mradi wa Boost
Katika kutekeleza mpango wa uboreshaji elimu ya msingi kupitia mradi wa BOOST, Tanga imepokea Shilingi 11,422,000,000. Kati ya hizi, Shilingi 6,766,100,000 zililenga ujenzi wa shule mpya 15, Shilingi 3,500,000,000 za ujenzi wa vyumba vya madarasa 140, Shilingi 760,100,000 za ujenzi wa madarasa 22 ya mfano ya elimu ya awali, Shilingi 25,000,000 kwa ajili ya ujenzi wa darasa 1 la watoto wenye mahitaji maalum.
Pia, Shilingi 370,800,000 zilitengwa kwa ujenzi wa matundu ya vyoo 177 na Shilingi 196,000,000 kwa ajili ya ujenzi wa nyumba 2 za walimu.
Golf Area/Masiwani Road Tanga
Anuani ya posta: P.O.Box 5095 Tanga
Simu: 027 2642421
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ras.tanga@tamisemi.go.tz
Haki miliki ©2017 Katibu Tawala Mkoa wa Tanga . Haki zote zimehifadhiwa.