Na Mashaka Mgeta, OMM TANGA
HATIMAYE mkoa wa Tanga umetangaza mpango wa kumuenzi nguli za fasihi, ndani na nje ya nchi, marehemu Shaaban Robert aliyezaliwa Januari Mosi, 1909 na kufariki dunia Juni 22, 1962.
Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Mhe Balozi Dk Batilda Burian, ameyasema hayo kwenye kongamano la kukumbuka kuzaliwa kwa Shaaban Robert, lililofanyika leo Januari 1, 2025 kwenye ukumbi wa ofisi ya Mkuu wa Mkoa.
Kongamano hilo limewajumuisha wazee, wakiwamo wenye simulizi za maisha na falsafa ya Shaaban Robert, watumishi wa umma, wajasiriamali na wanafunzi wa Shule ya Sekondari Pongwe walioghani mashairi mbalimbali yenye maudhui yanayofanana na malengo ya kongamano hilo.
Mhe Balozi Dk Batilda amesema sehemu ya mpango huo, inahusisha kuanzisha Shindano la Shaaban Robert kwa wanafunzi wa shule za msingi na sekondari, kisha kutoa zawadi kwa washindi ili kuchochea ari ya kuandika na kusoma vitabu, riwaya, mashairi na kuziishi falsasa za Shaaban Robert.
Amesema, mpango huo utahusisha pia kuendeleza kongamano hilo kila mwaka, kutafuta na kuhifadhi kwenye maktaba ya mkoa, nakala za vitabu, mashairi na maandishi mengine yaliyopo, vinavyotambulisha kazi za Shaaban Robert.
Mtafiti wa lugha, Bakari Nauma, amesoma wasifu wa marehemu Shaban Robert ‘uliogusia’, malezi katika familia, elimu na maeneo tofauti aliyofanya kazi ikiwemo idara ya forodha Pangani, alipokuza kipawa cha fasihi andishi, idara ya wanyamapori Mpwapwa na ofisi ya Mkuu wa Mkoa Tanga.
Mwalimu Musa Mayombe wa Shule ya Msingi Pongwe, anasema wapo wanafunzi wanaoshiriki nyanja mbalimbali zinazothibitisha kuwa na vipawa tofauti ikiwa ni pamoja na ushairi, hivyo ipo haja ya mpango kuwatambua na kuendeleza vipawa hivyo.
Golf Area/Masiwani Road Tanga
Anuani ya posta: P.O.Box 5095 Tanga
Simu: 027 2642421
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ras.tanga@tamisemi.go.tz
Haki miliki ©2017 Katibu Tawala Mkoa wa Tanga . Haki zote zimehifadhiwa.