• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali na Majibu |
    • Barua pepe |
Tanga Region
Tanga Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Tanga

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Dira na Dhima
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za maji
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
    • Idara
      • Utawala na Utumishi
      • Mipango na Uratibu
      • Miundombinu
      • Elimu
      • Afya
      • Maji
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Usimamizi wa Serikali za Mitaa
    • Vitengo
      • TEHAMA
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa ndani
      • Manunuzi
      • Sheria
  • Machapisho
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu za Maombi
    • Hotuba
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Sehemu ya picha
    • Habari
    • Matukio
  • Miradi
    • Miradi iliyokamilika
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya Pangani
    • Halmashauri ya Wilaya Mkinga
    • Halmashauri ya Wilaya Muheza
    • Halmashauri ya Jiji Tanga
    • Halmashauri ya Wilaya Korogwe
    • Halmashauri ya Mji Korogwe
    • Halmashauri ya Wilaya Handeni
    • Halmashauri ya Mji Handeni
    • Halmashauri ya Wilaya Kilindi
    • Halmashauri ya Wilaya Lushoto

TANZANIA, KENYA ZAZINDUA MAUNGANISHO YA MIKONGO YA MAWASILIANO

Imewekwa tarehe: July 19th, 2025

Na Mashaka Mgeta, MKINGA

TANZANIA na Kenya zimezindua Maunganisho ya Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano (NICTBB) wa Kampuni ya Simu (TTCL) unaotokea jijini Dar es Salaam na mikongo ya baharini iliyopo Mombasa, kupitia Mamlaka ya Habari na Mawasiliano (ICTA).

Hafla ya uzinduzi huo imefanyika jana Julai 18, 2025 kwenye eneo huru lililopo mpakani mwa nchi hizo, kati ya wilaya za Mkinga, Tanzania na Kaunti Kwale nchini Kenya imeongozwa na Waziri wa Teknolojia ya Mawasuliano, Mhe Jerry Silaa na Waziri wa Habari, Mawasiliano na Uchumi wa Kidijitali wa Kenya, Mhe William Kabogo.

Mhe Silaa amesema maunganisho hayo yataongeza kiwango cha upatikanaji wa mtandao wa uhakika, kupunguza gharama za matumizi ya mitandao na kuchochea ubunifu wa kidijitali kwa nchi hizo na ukanda wa Afrika Mashariki.

Amesema, uboreshaji teknolojia ya habari na mawasiliano ni miongoni mwa vipaumbele vya Mhe Rais Dkt Samia Suluhu Hassan vinavyoibua matokeo chanya yenye tija ikiwemo kuufikisha Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano  kwenye wilaya 109 ukiwa na urefu wa kilomita 13,820.

Mhe Silaa amesema, kwa mukhtadha huo, Tanzania inakwenda kufikia lengo la kuwa kitovu cha huduma za mawasiliano katika maeneo ya Mashariki na Kusini mwa bara ya Afrika.

Naye Mhe Kabogo amesema, maunganisho hayo si tu kwamba yatachochea mawasiliano, bali pia kuongeza ustawi wa biashara katika ukanda huo na Afrika kwa ujumla.

Amesema ufanisi wa maunganisho hayo utawafikia pia wafanyabiashara wadogo wakiwemo wanaofanya shughuli zao kwenye maeneo ya vijijini kama vile kwenye mpaka wa Horohoro, wadau wa sekta ya usafiri na usarishaji, miongoni mwa wengine wengi.

Mhe Kabogo amesema, matumizi ya teknolojia hiyo ya mawasiliano yanapaswa kutanuliwa ili kuyafikia maeneo mengine ya mipaka ya nchi hizo kama vile Sirari/Isibania, Namanga na Holili.

Viongozi wengine waliotoa salaam kwenye hafla hiyo na Mkurugenzi Mkuu wa TTCL, Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhandisi Leo Magomba, Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Tanga, Amina Saidi na Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Simu (TTCL), Moremi Marwa.

Kwa upande wa Kenya walikuwepo Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Mawasiliano na Uchumi wa Kidijitali, John Tanui, Kaimu Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia (ICTA), Zilfer Owiti, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya ICTA, Lily Ng’ok, Mbunge wa Kwale, Mangale Munga Chiforomodo.

Kwa nyakati tofauti, watendaji hao katika taasisi ya tasnia ya habari na mawasiliano, na wawakilishi wa wananchi, wameelezea azma yao ya kutekeleza majumu yanayolenga kuikuza sekta hiyo kupitia maunganisho ya mikongo iliyofanyika leo.

Matangazo

  • TANGA REGION INVESTMENT GUIDE November 24, 2023
  • SENSA YA WATU NA MAKAZI MWAKA 2022 MKOA WA TANGA June 13, 2023
  • Angalia zote

Habari mpya

  • TANZANIA, KENYA ZAZINDUA MAUNGANISHO YA MIKONGO YA MAWASILIANO

    July 19, 2025
  • WAANDISHI DODOMA WAVUTIWA NA MAENDELEO YA TANGA, WAALIKWA KUFANYA ZIARA

    July 17, 2025
  • RC BATILDA:ONGEZEKO LA WATU TANGA ISHARA YA UBORA WA HUDUMA ZA FYA, USTAWI WA JAMII

    July 17, 2025
  • TANGA TUNA UTOSHELEZI WA CHAKULA - BALOZI BATILDA

    July 17, 2025
  • Angalia zote

Video

KATIBU TAWALA MKOA WA TANGA AKIONGOZA WATUMISHI WA MKOA HUO KUFANYA MAZOEZI YA PAMOJA KATIKA UWANJA WA MKWAKWANI KUITIKIA WITO WA MHE. MAKAMU WA RAIS
Video zaidi

Viunganishi vya haraka

Tovuti zinazoendana

  • TAMISEMI
  • Kupata huduma za kiutumishi
  • Wakala ya Serikali Mtandao
  • Utumishi
  • Baraza la Mitihani Tanzania (NECTA)
  • Tovuti ya Serikali

Kifuatilia watazamaji duniani

world map hits counter

idadi ya watazamaji

free HitCounter

Ramani ya Mkoa wa Tanga

Wasiliana nasi

    Golf Area/Masiwani Road Tanga

    Anuani ya posta: P.O.Box 5095 Tanga

    Simu: 027 2642421

    Simu ya Mkononi:

    Barua pepe: ras.tanga@tamisemi.go.tz

Anuani zingine

   

    • Sera za faragha
    • Kanusho
    • Maswali na Majibu
    • Ramani ya Tovuti
    • Huduma

Haki miliki ©2017 Katibu Tawala Mkoa wa Tanga . Haki zote zimehifadhiwa.