Na Mashaka Mgeta, OMM TANGA
VIJANA wametakiwa kutumia stadi bunifu zinazojikita katika misingi ya kizalendo kwa taifa, ili kuibua shughuli, miradi ama huduma zitakazowawezesha kupata kipato, na hivyo kuondokana na athari zinazotokana na ukosefu wa ajira.
Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Mhe Balozi Dk Batilda Burian, ameyasema hayo leo Novemba 25, 2024, alipozungumza na Balozi wa Mazingira na Uhamasishaji, Michael Msechu aliyefika ofisi kwake kumuaga, baada ya kuhitimisha ziara kwenye wilaya nane za mkoa huo.
Amempongeza Msechu kwa kujitolea kwake kuhamasisha umma kuhusu umuhimu wa hifadhi ya mazingira, kazi inayomfikisha kwenye maeneo tofauti ya nchi, akiielimisha na kuihamasisha jamii kuhusu umuhimu na faida za hifadhi ya mazingira.
Mhe Balozi Dk Batilda amesema haistahili kwa vijana kusubiri mafanikio yasiyotokana na jitihada zao, hivyo ubunifu na kujituma vinapaswa kuwa nyenzo za kuwaongoza katika kufikia malengo yao.
Naye Msechu amesema pamoja na elimu na hamasa kuhusu hifadhi ya mazingira, amezungumza na vijana na kuwashirikisha namna tofauti za kujiendeleza na kulitumikia taifa.
Pia amesema amekutana na wananchi walioelezea kuridhishwa na namna Serikali ya Mhe Rais Dk Samia Suluhu Hassan, inavyotekeleza ahadi zake kwa kuanzisha na kuendeleza miradi katika sekta mbalimbali zinazogusa maendeleo na ustawi wa watu.
Vijana walioteuliwa kuunda timu za kuendeleza ari ya hifadhi ya mazingira kutoka wilaya za mkoani humo, wamesema ziara ya Msechu imekuwa yenye manufaa kwao.
Golf Area/Masiwani Road Tanga
Anuani ya posta: P.O.Box 5095 Tanga
Simu: 027 2642421
Simu ya Mkononi:
Barua pepe: ras.tanga@tamisemi.go.tz
Haki miliki ©2017 Katibu Tawala Mkoa wa Tanga . Haki zote zimehifadhiwa.