• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali na Majibu |
    • Barua pepe |
Tanga Region
Tanga Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Tanga

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Dira na Dhima
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za maji
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
    • Idara
      • Utawala na Utumishi
      • Mipango na Uratibu
      • Miundombinu
      • Elimu
      • Afya
      • Maji
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Usimamizi wa Serikali za Mitaa
    • Vitengo
      • TEHAMA
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa ndani
      • Manunuzi
      • Sheria
  • Machapisho
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu za Maombi
    • Hotuba
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Sehemu ya picha
    • Habari
    • Matukio
  • Miradi
    • Miradi iliyokamilika
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya Pangani
    • Halmashauri ya Wilaya Mkinga
    • Halmashauri ya Wilaya Muheza
    • Halmashauri ya Jiji Tanga
    • Halmashauri ya Wilaya Korogwe
    • Halmashauri ya Mji Korogwe
    • Halmashauri ya Wilaya Handeni
    • Halmashauri ya Mji Handeni
    • Halmashauri ya Wilaya Kilindi
    • Halmashauri ya Wilaya Lushoto

WATAHINIWA 65,955 WAANZA MITIHANI

Imewekwa tarehe: September 14th, 2023


Na Emma Kigombe






Watahiniwa  wapatao 65, 955 wameanza mitihani yao ya kuhitimu Elimu ya msingi katika mkoa wa Tanga ambapo kati ya waliosajiliwa wavulana ni 30,831 na wasichana 35,145.


Jumla ya Shule zilizosajikiwa ni 1057 ambapo shule za Serikali ni 996 na binafsi ni 61 katika Halmashauri zote 11 za mkoa wa Tanga.


Akizungumza Afisa Elimu wa mkoa wa Tanga Newaho Mkisi amesema mkoa wa Tanga umejipanga vizuri kuhakikisha mitihani inafanyika pasipo kikwazo chochote.


Newaho amewataka wote wanaohusika  na usimamizi wa mitihani hiyo kufanya kazi kwa bidii huku wakizingatia uwaninifu na kuepuka vitendo vitakavyoweza kuharibu mitihani hiyo.


"Waalimu tutakaohusika na kazi hii maalumu nawakumbusha tufanye kazi kwa bidii na umakini mkubwa tukizingatia uadilifu huku tukijiepusha na vitendo ambavyo vinaweza kuharibu mitihani kwa kuwa Serikali haitafumbia macho kwa mtu yoyote atakayefanya udanganyifu au kuharibu zoezi zima la mitihani" alisema afisa Elimu


Sambamba na hilo amewataka wanafunzi kutulia na kujiamini  kwa kuwa wamefanya maandalizi ya kutosha kufanya mtihani huo.


"Kwa miaka saba tumeshajifunza mengi, tumeweza kukamikisha mada, tumefanya mazoezi ya kutosha ninaamini kupitia mitihani iliyokuwa inafanyika mara kwa mara watafanya vizuri na kufahulu" aliongeza afisa Elimu.


Mitihani ya kuhitimu Elimu ya msingi inafanyika kwa siku mbili tarehe 13 na 14 nchini kote.





Matangazo

  • TANGA REGION INVESTMENT GUIDE November 24, 2023
  • SENSA YA WATU NA MAKAZI MWAKA 2022 MKOA WA TANGA June 13, 2023
  • Angalia zote

Habari mpya

  • SARUJI TANGA YAKABIDHI BAJAJI ZA UMEME 10 KWA BALOZI BATILDA

    July 03, 2025
  • RC TANGA ASULUHISHA MGOGORO WA ARDHI TAFSIRI HASI YA RAMANI IKITAJWA CHANZO

    July 03, 2025
  • RAS MCHATTA: SINA MANENO MENGI, NIPIMENI KWA KAZI, UWAJIBIKAJI

    June 30, 2025
  • BALOZI BATILDA AAGIZA WAKUU WA WILAYA KUSIKILIZA KERO, AWAAPISHI WAWILI TANGA

    June 30, 2025
  • Angalia zote

Video

KATIBU TAWALA MKOA WA TANGA AKIONGOZA WATUMISHI WA MKOA HUO KUFANYA MAZOEZI YA PAMOJA KATIKA UWANJA WA MKWAKWANI KUITIKIA WITO WA MHE. MAKAMU WA RAIS
Video zaidi

Viunganishi vya haraka

Tovuti zinazoendana

  • TAMISEMI
  • Kupata huduma za kiutumishi
  • Wakala ya Serikali Mtandao
  • Utumishi
  • Baraza la Mitihani Tanzania (NECTA)
  • Tovuti ya Serikali

Kifuatilia watazamaji duniani

world map hits counter

idadi ya watazamaji

free HitCounter

Ramani ya Mkoa wa Tanga

Wasiliana nasi

    Golf Area/Masiwani Road Tanga

    Anuani ya posta: P.O.Box 5095 Tanga

    Simu: 027 2642421

    Simu ya Mkononi:

    Barua pepe: ras.tanga@tamisemi.go.tz

Anuani zingine

   

    • Sera za faragha
    • Kanusho
    • Maswali na Majibu
    • Ramani ya Tovuti
    • Huduma

Haki miliki ©2017 Katibu Tawala Mkoa wa Tanga . Haki zote zimehifadhiwa.