• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • Maswali na Majibu |
    • Barua pepe |
Tanga Region
Tanga Region

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Tanga

  • Mwanzo
  • Kuhusu sisi
    • Dira na Dhima
  • Huduma
    • Huduma za Afya
    • Huduma za maji
  • Utawala
    • Muundo wa Sekretarieti ya Mkoa
    • Idara
      • Utawala na Utumishi
      • Mipango na Uratibu
      • Miundombinu
      • Elimu
      • Afya
      • Maji
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Usimamizi wa Serikali za Mitaa
    • Vitengo
      • TEHAMA
      • Fedha na Uhasibu
      • Ukaguzi wa ndani
      • Manunuzi
      • Sheria
  • Machapisho
    • Taratibu
    • Taarifa
    • Sheria
    • Fomu za Maombi
    • Hotuba
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Sehemu ya picha
    • Habari
    • Matukio
  • Miradi
    • Miradi iliyokamilika
  • Halmashauri
    • Halmashauri ya Wilaya Pangani
    • Halmashauri ya Wilaya Mkinga
    • Halmashauri ya Wilaya Muheza
    • Halmashauri ya Jiji Tanga
    • Halmashauri ya Wilaya Korogwe
    • Halmashauri ya Mji Korogwe
    • Halmashauri ya Wilaya Handeni
    • Halmashauri ya Mji Handeni
    • Halmashauri ya Wilaya Kilindi
    • Halmashauri ya Wilaya Lushoto

WAZIRI KIJAJI AHIMIZA MALEZI BORA KWA WATOTO

Imewekwa tarehe: January 9th, 2025

Na Mashaka Mgeta, KOROGWE

WAZIRI wa Mifugo na Uvuvi, Mhe Dk Ashatu Kijaji, amewahimiza wazazi na walezi, kutilia mkazo malezi bora yanayowajenga watoto kimaadili, ili kuwa na kizazi chenye tija kwa maendeleo endelevu wan chi.

Mhe Dk Kijaji amesema, fedha nyingi zinazotolewa na Serikali ya Rais Dk Samia Suluhu Hassan kwa ujenzi wa miundombinu na huduma katika sekta mbalimbali ikiwemo elimu, haitakuwa na maana kama watoto watakua katika mmomonyoko wa maadili, na hivyo kushindwa kuwa na stadi na maarifa yanayowastahili.

Mhe Dk Kijaji ametoa rai hiyo kwa nyakati tofauti na leo Januari 9,2025, alipotembelea shule za sekondari za Lunguza na Rashid Shangazi (Lushoto), Nyerere, Semkiwa, Makorola na Foroforo wilayani Korogwe.

Amesema sekta ya elimu ni miongoni mwa maeneo ya vipaumbele kwa Rais Dk Samia, hivyo kuwekeza fedha nyingi kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu, ili kuwepo na elimu bora kwa kila mtoto wa kitanzania.

Hata hivyo, amesema nia njema hiyo ya Mhe Rais Dk Samia, inapaswa kuendana na utayari wa wazazi na walezi, kuwalea watoto katika misingi ya maadili mema, na kuepuka kuwaita majina yasiyofaa kama vile ‘Watoto wa Siku Hizi’.

‘’Hawa ni watoto wetu, mnapowaita ‘Watoto wa Siku Hizi’ huyo ‘Siku Hizi’ ni nani,’’anahoji Mh Dk Kijaji.

Pia, Mhe Dk Kijaji amewaasa watoto waliopo mashuleni, kusoma kwa bidii na kujiepusha na vitendo vinavyochangia kuwaathiri kwa namna tofauti na hatimaye kuwakatisha masomo.

Amesema kupata na kuhitimu elimu bora kunachangia kuwajengea uwezo na maarifa watoto kuwa viongozi bora wa baadaye, akitoa mfano wa Mhe Rais Dk Samia.

‘’Mkiwa wasikivu na watiifu kwa wazazi na walezi wenu, mkiwasikiliza walimu na kufuata na kuyashika wanayowafundisha, mtapata manufaa bora zaidi kwa baadaye,’’ ameasa.

Akiwa wilayani Korogwe leo, Mhe Dk Kijaji ametembelea, kukagua na kuweka mawe wa msingi kwenye miradi yenye thamani ya jumla ya Shilingi 1,820,880,029.

Miradi hiyo na thamani ya kila mmoja kwenye mabano ni madarasa matano na matundu nane ya vyoo katika Shule ya Sekondari Nyerere (139,400,000), madarasa matatu na matundu nane ya vyoo katika Shule ya Sekondari Semkiwa (89,400,000).

Mingine ni shule mpya ya sekondari Makorola (584,280c,29), nyumba ya Afisa Ugani katika kata ya Magoma (40,000,000) na miundombinu ya madarasa, nyumba ya walimu, matundu ya vyoo na mabweni Shule ya Sekondari Foroforo (739,000,000).

Matangazo

  • TANGA REGION INVESTMENT GUIDE November 24, 2023
  • SENSA YA WATU NA MAKAZI MWAKA 2022 MKOA WA TANGA June 13, 2023
  • Angalia zote

Habari mpya

  • RAS MCHATTA: SINA MANENO MENGI, NIPIMENI KWA KAZI, UWAJIBIKAJI

    June 30, 2025
  • BALOZI BATILDA AAGIZA WAKUU WA WILAYA KUSIKILIZA KERO, AWAAPISHI WAWILI TANGA

    June 30, 2025
  • RC BATILDA ATAKA MAADILI, UTAWALA BORA KUIMARISHWA SERIKALINI

    June 25, 2025
  • MIAKA MINNE, SIKU 23 ZA RAS MNYEMA TANGA, AHAMISHIWA PWANI

    June 24, 2025
  • Angalia zote

Video

KATIBU TAWALA MKOA WA TANGA AKIONGOZA WATUMISHI WA MKOA HUO KUFANYA MAZOEZI YA PAMOJA KATIKA UWANJA WA MKWAKWANI KUITIKIA WITO WA MHE. MAKAMU WA RAIS
Video zaidi

Viunganishi vya haraka

Tovuti zinazoendana

  • TAMISEMI
  • Kupata huduma za kiutumishi
  • Wakala ya Serikali Mtandao
  • Utumishi
  • Baraza la Mitihani Tanzania (NECTA)
  • Tovuti ya Serikali

Kifuatilia watazamaji duniani

world map hits counter

idadi ya watazamaji

free HitCounter

Ramani ya Mkoa wa Tanga

Wasiliana nasi

    Golf Area/Masiwani Road Tanga

    Anuani ya posta: P.O.Box 5095 Tanga

    Simu: 027 2642421

    Simu ya Mkononi:

    Barua pepe: ras.tanga@tamisemi.go.tz

Anuani zingine

   

    • Sera za faragha
    • Kanusho
    • Maswali na Majibu
    • Ramani ya Tovuti
    • Huduma

Haki miliki ©2017 Katibu Tawala Mkoa wa Tanga . Haki zote zimehifadhiwa.